Na Denis Chambi, Tanga.

MDHAMINI Ligi kuu ya soka Tanzania bara Benki ya NBC  imeeleza shauku yao ya kutaka kuendelea kuupa thamani  mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini ambapo imeanza mazungumzo na baadhi  vilabu ili kuwajenga viwanja vya mazoezi ikiwa ni sehemu ya ajenda yao katika sekta ya michezo.

Akizungumza Mkoani Tanga wakati wa kukabidhi gari la Klabu ya Coastal Union Kaimu Mkurugenzi wa benk ya NBC Alvis Ndunguru  ameeleza pamoja na  kuzisadia timu kwenye eneo la usafiri   bado  zinakabiliwa na ukosefu wa miundombinu ya viwanja hivyo kupitia ajenda yao ya michezo wanakwenda kuboresha eneo hilo ambalo litakuwa na tija kwa timu Klabu katika kuwaongezea mapato.

"Miundombinu ya viwanja ipo pia kwenye ajenda yetu  ipo nafasi ya mazungumzo  na sisi kama NBC tutaendelea kuwekeza  kwenye eneo la miundombinu ya viwanja, lakini pia tumewekeza kwenye kadi za uwanachama zipo Klabu tumeshirikiana nazo  tunajua kadi ni sehemu nzuri kwa Klabu kuongeza mapato sisi tutaendelea kushirikiana na klabu zote" alisema.

Akizungumzia uwekezaji walioufanya katika sehemu ya usafiri kwa klabu za ligi kuu hapa nchini amesema kuwa mpaka sasa benk hiyo imetumia kiasi cha shilingi Bilion 1.3 kuzipatia usafiri timu za  KMC, Singida Black Stars, Namungo  pamoja na Coastal Union.

"Sisi kama Benki ya NBC tunaona michezo ni sehemu kubwa na tumewekeza kwa kiwango kikubwa kwa ujumla kwenye ligi kuu tumewekeza shilingi Bilion 32.6 katika mkataba tulionao katika kuendelea michezo Tanzania hasa mpira wa miguu"

"Tunaelewa vilabu vimekuwa vikipata changamoto mbalimbali hasa za usafiri katika kuboresha eneo hili  mpaka sasa  tumetoa mabasi 4 kwa vilabu vinne vya Coastal Union, Namungo, Singida black stars pamoja na KMC huu ni uwekezaji katika ligi ya nne kwa ubora barani Afrika na tutaendelea kuwekeza zaidi katika eneo hili, tukichukua eneo la mabasi peke yake tumekwisha wekeza takribani Bilion 1.2 hadi sasa" alisema Ndunguru 

Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union Muhsin Hassan amesema kuwa kiu ya muda mrefu waliokuwa nayo mashabiki wapenzi na wanachama wa Coastal Union  juu ya kumiliki usafiri wait sasa umepata mwarobaini.

"Tumshukuru sana Benki ya NBC kwa kutusaidia kupata usafiri, suala hili la usafiri lilikuwa ni tatizo kubwa sana kwetu japo kuwa tulishawahi kuwa na usafiri lakini ulikuwa haukidhi  mahitaji yetu"alisema Muhsin.

Akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Tanga katika hafla hiyo ya kukabidhi gari kwa Klabu ya Coastal Union Mkuu wa wilaya ya Lushoto Zephania Sumaye ameitaka kalabu hiyo kuhakikisha inaendelea kufanya vizuri kwenye ligi ili kuuwakilisha vyema mkoa huo katika michuano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu, utawala bora .

"Tunatamani tuone mafanikio haya yanaendana na matokeo mazuri ya timu tunawapongeza kuwepo ligi kuu lakini tunatamani mpige hatua zaidi na hii italetwa na utawala bora,  miundombinu bora ya kimichezo, mazingira bora ya kifedha na nidhamu ya wachezaji ambao wataisaidia kuchangia mabadiliko chanya katika timu mna nafasi ya kuifanya timu ya Coastal Union kuwa bora zaidi"alisisitiza Sumaye
Share To:

Post A Comment: