Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla maalum ya Iftar iliyoandaliwa na Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) kwa kushirikiana na Benki mbalimbali iliyofanyika ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.

Awali amelipongeza Shirika la Bima Zanzibar kwa kuumarika kama mgeni rasmi na kwamba Shirika hilo linatoa mchango mkubwa nchini sanjari na kukuza uchumi hususani katika uongozi wa Serikali ya awamu ya nane ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inayoongozwa na Rais Dkt Hussein Ally Mwinyi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Aidha Serikali itaendelea kuimarisha huduma za Bima na mifumo ya fedha kidijitali ili kuwanufaisha wananchi wake.

Kwa niaba ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mahundi amesema Serikali inaendelea kuboresha mifumo ya bima na kifedha ili kuendana kidijitali sanjari na kutoa bima za mikopo.








Share To:

Post A Comment: