Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi katika maadhimisho ya wiki ya wanawake amefanya matendo ya huruma kwa wahitaji Wilayani Chunya hafla iliyofanyika ukumbi wa Sapanjo.

Kutika hafla hiyo Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amekabidhi kiti mwendo kwa mtoto mwenye uhitaji,vifaa vya shule kwa watoto wenye mahitaji maalumu na wazee.

Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema yeye kama Mbunge wa Viti Maalumu kiu yake ni kuona watu wenye mahitaji nao wanaishi mazingira rafiki.

Awali wanawake walitembelea wadi ya wazazi katika hospitali ya Wilaya ya Chunya.












Share To:

Post A Comment: