Kamati Kuu ya Chama cha Wandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya (Mbeya Press Club - MBPC) imewataka Waandishi wa Habari wote wa Mkoa huo kutoshiriki shughuli za Chama cha Mapinduzi (), mpaka Kamati Kuu ya CCM itakapomaliza tofauti za pande zote mbili ikiwemo kuwalipa fedha wanazodai tangu Februari 7, 2024 

Taarifa ya MBPC imeeleza Hati ya Madai iliwasilishwa baada ya makubaliano ya pande hizo mbili, Madai hayo ni posho za Waandishi walioshiriki kwenye ziara ya Siku 2 ya aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Paul Makonda

Wameeleza Mwandishi yeyote ambaye atashiriki kwenye shughuli za Chama hicho, atachukuliwa hatua za kinidhamu pamoja na kutoshiriki kwenye tatizo lolote ambalo litamkuta na kuwa Waraka huo ni kwa Waandishi wote bila kujali ni Wanachama au si Wanachama wa klabu hiyo

Share To:

Post A Comment: