Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akipata maelezo kuhusiana ubunifu wa vazi la bibi harusi linalobuniwa na mtanzania kwenye kongamano la mavazi na ngozi kuelekea maadhimisho ya miaka 30 ya VETA.
Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akipata maelezo kuhusiana kwa vijana wenye ulemavu wakionesha ujuzi wao kushona nguo kwenye kongamano la mavazi na ngozi kuelekea maadhimisho ya miaka 30 ya VETA.

Matukio katika picha kwenye kongamano la Mavazi ,Ngozi kuelekea maadhimisho ya miaka 30 ya VETA.
Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akizungumza kwenye kongamano la mavazi na ngozi kuelekea maadhimisho ya miaka 30 ya VETA.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore akizungumza kuhusiana na VETA ilivyojipanga katoa mafunzo nchini kwenye kongamano la mavazi na ngozi kuelekea maadhimisho ya miaka 30 ya VETA.
Mbunifu wa Mavazi Mstapha Hassanal akizungumza kuhusiana na ubunifu wa mavazi kwenye kongamano la mavazi na ngozi kuelekea maadhimisho ya miaka 30 ya VETA.
Na Chalila Kibuda
SERIKALI imesema kuwa katika kuandaa vijana katika masuala ya ubunifu na ujuzi kunahitaji kuimarisha ushirikiano baina ya viwanda na wazalishaji katika kuongeza uwanja wa ajira kwa vijana wanaopata mafunzo ya ujuzi na Ufundi Stadi.
Hayo ameyasema Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda katika Kongamano na Wadau wa Sekta ya Nguo na Mavazi lililoandaliwa na Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kuelekea maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Mamlaka hiyo.
Amesema kuwa mashirikiano kati ya VETA na Wazalishaji na Viwanda kunajenga kuelewa soko la bidhaa walizobuni au kufanya kazi na wadau hao wakiwemo wazalishaji mbalimbali wakiwemo wa magari ,viwanda vya nguo,wabunifu, mavazi pamoja na sekta ya ujenzi
“Tunataka kuona ushirikiano wa kampuni za ujenzi na VETA, ujenzi wa nyumba nzuri na hivi sasa ujenzi wa nyumba nzuri unaenda kasi sana ambapo vijana wetu wanatakiwa kushiriki huko moja kwa moja na kujua mahitaji yao,” amesema.
Profesa Mkenda amesema kuna wabunifu wapo na hawana elimu ya ufundi ambao wanafanya vizuri hivyo wanachokifanya wanatakiwa wafundishe vijana wanaopata mafunzo ya ujuzi na ufundi.
Profesa Mkenda amesema wadau ambao wako sokoni wanatakiwa kuingia katika madarasa na kufundisha wanachokijua kwenye soko na kutoa mwanga kwa wanafunzi pindi wanapohitimu kuwa na uwanja mpana wa ajira.
Hata hivyo amesema kongamano hilo ndio maagizo yake ili kuleta picha ya mahitaji yaliyopo sokoni kutokana wadau kutoa mawazo yao.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Wilson Mahera amesema kuwa kinachofanyika katika kongamano hilo ni maelekezo ya Waziri Profesa Mkenda
Amesema kuwa katika utoaji wa mafunzo wanaangalia kuboresha sera ambayo itaendana na wakati uliopo kwenye mafunzo hayo.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore amesema kwenye eneo la ujuzi wana jukumu la kufundisha ujuzi kutokana na mahitaji yaliyopo kwenye soko la ajira.
Amesema kwa kuthamini ujuzi serikali inahakikisha vyuo vya ufundi vinakuwepo vya kutosha, ndio maana vipo zaidi ya 800 nchini.
“Maana yake ni sekta ambayo watu wengi wanahitaji kupata ujuzi,” amesema.
Post A Comment: