Magari matatu yamekabidhiwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda na Musoma Dc Mkoani mara na Shirika la Amrefu Tanzania kwaajili ya ufatiliaji na utoaji wa huduma kwa wananchi huku madereva wakionywa kuacha kubeba vitu visivyositahili.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa mara Gelard Kusaya Wakati wa kupokea magari hayo kutoka kwa Meneja miradi wa shirika Amrefu Tanzania DKT Recotus Masanja ambapo alisema magari hayo nikuimarisha ufatiliaji wa huduma za Afya kwa Wananchi.

Kusaya amewaonya madereva kuacha kupakua vitu visivyositahili katika magari hayo badala yake yatumike kama ilivyokusudiwa.

Kwa upande wake Mganga Mkuu Mkoa wa Mara Zabron Masatu Alisema kupatikana kwa magari hayo kusaidia kuondoa changamoto ya ukosefu wa magari huku Meneja miradi wa Amref amesema magari hayo yameyatoa ili kusaidia utoaji wa huduma kwa wananchi.







Share To:

Post A Comment: