Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera na Uratibu, William Lukuvi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa wameungana na familia na waumini kushiriki Misa Takatifu ya kumuombea Rais wa awamu ya Tano, Hayati Dkt. John P. Magufuli, leo tarehe 17 Machi 2025.
Misa hiyo Takatifu imeongozwa na Mhashamu Baba Askofu Severine Niwemugizi, Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara katika Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Yohana Maria Muzeyi Mlimani wilayani Chato mkoa wa Geita.
Misa hiyo Takatifu ya kumuombea aliyekuwa Rais wa awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Magufuli inafanyika ikiwa imetimia miaka minne tangu alipofariki dunia Machi 17, 2021.
Familia ya Hayati Magufuli ikiongozwa na Mke wa Hayati Dkt. Magufuli, Mama Janeth Magufuli, Watoto wa Hayati, Wanafamilia, ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wa Mkoa Geita wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Geita, Martine Shigela wameshiriki katika Misa hiyo.
Post A Comment: