Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeridhishwa na ufanisi na ubora wa majengo ambayo yanaendelea kujengwa ndani ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kupitia mapato ya ndani kwa kutumia wataalam wa ndani yaani mfumo wa ‘Force Account’
Akizungumza katika ziara ya kikazi ya kamati hiyo Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Japhet Hasunga (MB) ameupongeza Uongozi wa Chuo kwa ujenzi huo ambao amesema umetumia gharama nafuu, majengo yamejengwa katika viwango bora na kuonesha thamani ya fedha kwenye miradi hiyo.
“Tumetembea sehemu nyingi tumeona wengi wao wameshindwa kutumia vizuri mfumo wa huu lakini hapa mmefanikiwa kwa hilo ninawapongeza sana na muendelee hivyo hivyo, Amesema Mhe. Hasunga
Mhe. Hasunga ameongeza kuwa IAA imekuwa Chuo cha mfano kutokana jitihada zinazofanyika katika kuboresha na kuongeza miundombinu ili kuendana na mipango yake ya kuongeza wanafunzi ambapo kwa mwaka huu wa masomo kuna zaidi ya wanafunzi 17,000 katika kampasi zake hapa nchini ikiwemo Arusha, Dar es salaam, Dodoma, Babati na Songea
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Aruaha(IAA)Prof. Eliamani Sedoyeka amesema miongoni mwa masuala yaliyochangia IAA kufanikiwa katika matumizi ya mfumo wa Force Account ni usimamizi wa karibu, uwajibikaji wa watalaam na kujitoa kwa kila mtaalam katika utekelezaji wa miradi.
Aidha, Prof. Sedoyeka ameongeza kuwa IAA imeunda kamati zinazosimamia miradi na kamati hizo zina mahitaji yote ya wataalam wanaopaswa kuwepo katika utekelezaji wa mradi, “Sisi IAA tuna Kamati ya Force Account na chini yake zipo kamati ndogo ndogo za wataalam,, kamati hizo zina wataalam wote ambao hata kama ni mkandarasi angetekeleza miradi hii angekuwa nao”.
Awali akiwasilisha taarifa ya miradi hiyo Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi IAA Dkt. Daniel Shayo amesema miradi hiyo ilianza mwezi Januari 2021 na inategemewa kukamilika mwezi Juni mwaka huu na imegharimu kiasi cha Jumla ya Sh. Billion 24
Naye Mjumbe wa kamati hiyo Mbunge wa jimbo la Momba Mhe. Kondesta Sichalwe (MB) amejivunia kusoma wa IAA na kusisitiza Elimu aliyoipata inaishi kwani ndio iliyompa nafasi aliyonayo kwa sasa hivyo ametoa rai kwa watanzania kuifanya IAA chaguo la kwanza katika masomo ya Elimu ya kati na Elimu ya juu.
Post A Comment: