Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeupongeza Mfuko wa Jamii kwa Watumishi wa Umma(PSSSF) kwa kusimamia uwekezaji wenye tija katika miradi ya maendeleo na utoaji huduma bora kwa wanachama.
Mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma (PSSSF), umewaondolea wasiwasi wastaafu wa mfuko huo kufuatia kuendelea kukua na kukaribia kufikia thamani ya Trilioni 10 na hivyo kuwahakikishia kuendelea kupata mafao yao kwa wakati.
Hayo yameelezwa jana jijini hapa na Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa PSSSF, Abdulrazaq Abdu alipokuwa akitoa taarifa ya mradi wa nyumba wa PSSSF Olorieni kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii iliyokuwa imetembelea mradi huo.
Kufuatia taarifa hiyo kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeupongeza Mfuko huo wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa jinsi inavyosimamia vitega uchumi vyake ambavyo kwa sasa vinajiendesha kwa faida.
Kauli hiyo imetolewa na wajumbe mbalimbali wa kamati hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Bi. Fatma Taufiq Machi 12, 2025 jijini Arusha wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi wa makazi wa Olorien.
“Kwa kweli nawapongeza PSSSF kwa kusimamia vyema mradi huu ambao tumeelezwa kuwa umeshaanza kuingiza faida, hongereni sana. Hata hivyo pongezi za dhati kabisa ziende kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa miongozo bora iliyowezesha PSSSF kusimamia vyema mradi huu na mingine yote” alisema Mhe. Taufiq.
Mwenykiti huyo wa kamati hiyo ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii aliipongeza PSSSF kwa kulipa kwa wakati mafao ya wanachama ukilinganisha na siku za nyuma, alisema hivi sasa hakuna mlalamiko mengi ya wanachama wakilalamikia mafao kutoka PSSSF.
“Pia kwa niaba ya kamati nawapongeza kwa utuzaji mzuri wa fedha za wanachama, kwa kuwekeza vyema katika maeneo yanayolipa, endeleeni hivyohivyo” alisema Mwenyekiti huyo.
Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Ridhiwani Kikwete, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu alisema, “Tumepokea maelekezo na ushauri wa kamati, tunayachukua na tunaahidi kutafanyia kazi ili tuweze kupata faida ya uwezaji ya Mfuko”.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu, Bw. Abdul-Razaq Badru alisema uhimilivu wa Mfuko upo vizuri na thamani ya Mfuko inazidi kuongezeka na sasa tunawalipa wanachama wetu kwa wakati na usahihi. Pia alisema miradi mingi ya Mfuko inaendeshwa kwa faida.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, ipo katika ziara kutembelea miradi mbalimbali ya taasisi za umma ili kujionea uendeshwaji wa miradi hiyo.
Post A Comment: