Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Arusha Simon Maximillian Iranghe amewataka vijana Wilayani Arumeru kugombea nafasi za nyazifa mbalimbali za uongozi ili kuweza kuisemea serikali vyema kupitia miradi mbalimbali ya kimaendeleo iliyotekelezwa na inayotekelezwa katika sehemu mbalimbali za nchi hii.
Simon Iranghe ameyasema hayo katika ziara ya Kamati ya utekelezaji ya Uvccm mkoa wa Arusha iliyofanyika Wilayani humo ya kukagua uhai wa Jumuiya hiyo sambamba na kukutana na makundi mbalimbali ya vijana wakiwemo madereva wa bodaboda,vijana na shirikisho pamoja na wanufaika wa mikopo ya halmashauri ya asilimia 10.
Akizungumza na vijana hao Mwenyekiti huyo amewaonya vijana hao kuacha tabia ya kutengenezeana chuki na ajali katika kipindi hiki ambacho kunatarajiwa kufanyika uchaguzi mkuu.
Ameongeza kuwa kwasasa jamii imeingia katika changamoto kubwa ya kijinsia ya kupotea kwa vijana kutokana na mmomonyoko wa maadili na ukatili wa kijinsia unaoendelea kufanyika kwenye jamii hivyo amewataka vijana hao kutumia nafasi zao kukemea vitendo hivyo viovu.
Sambamba na hilo mwenyekiti huyo amempongeza kada ya chama cha mapinduzi Jonhson Exaud Sarakikya kwa kutoa matofali 1000 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba wa Katibu wa vijana wa Wilaya hiyo kwani kukamilika kwa nyumba ya mtumishi huyo kutasaidia kuondoa changamoto ya makazi.
Naye Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (VCCM) Taifa na Mbaraza Mkoa wa Aruasha Tezra Furaha Semuguruka amesema kuwa lengo la ziara hiyo ni kuwahamasisha vijana kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa utakaofanyika oktoba 2025.
"Ila niwaombe Vijana wenzangu mgombea atakayesimamishwa na Chama chetu CCM kupeperusha bendera tuungane kwa pamoja kwenda kuhakikisha anapata ushindi wa kishindo wa CCM,hivyo vijana tusilale mpaka kieleweke" Aliongezea Tezra
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Meru Ombeni Pallangyo amesema kama vijana wa Meru watafanya kazi za chama cha mapinduzi na siyo kubeba mikoba ya watu ili kuhakikisha Chama hicho kinasonga mbele.
Hata hivyo Pallangyo amewataka vijana wa meru kuacha tabia ya kubeba mabegi ya wagombea badala yao nao wajitokezekugombea katika nafasi za udiwani na ubunge ili kuongeza wigo mpana wa vijana kuingia katika vyombo vya maamuzi.
Post A Comment: