
Afisa Usimamizi wa Sekta ya Fedha Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Wizaya ya Fedha, Bw. Santley Kibakaya, akitoa elimu ya fedha kwa Wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Musoma, mafunzo ya elimu ya fedha yalitolewa na Wizara ya Fedha, pamoja na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), TCB, NMB, CRDB na NBC, mkoani Mara.

Afisa Msimamizi wa Fedha Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha Bi. Elizabeth Mzava, akigawa kipeperushi chenye taarifa kuhusu uwekaji akiba kwa Bw. Zakayo Emmanuel, mkazi wa Busekera, mkoani Mara, wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wizara ya Fedha, pamoja na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), TCB, NMB, CRDB na NBC.

Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Musoma, Bi. Jacqueline Wanzagi, akimkabidhi zawadi ya fulana, Bi. Ester Tingali, baada ya kujibu swali kuhusu umuhimu wa kusoma mkataba kabla ya kusaini kuchukua mkopo, wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wizara ya Fedha, pamoja na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), TCB, NMB, CRDB na NBC mkoani Mara.

Baadhi ya watumishi wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB) wakifuatilia mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa kwa Wananchi mkoani Mara, na Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), NMB, CRDB, NBC na Benki hiyo.

Baadhi ya watumishi wa Benki ya CRDB, wakifuatilia mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa kwa Wananchi mkoani Mara, na Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), TCB, NMB, NBC na CRDB.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha wakisoma vipeperushi vyenye taarifa mbalimbali wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wizara ya Fedha, pamoja na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), TCB, NMB, CRDB na NBC, mkoani Mara.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha wakazi wa Kijiji cha Busekera, wakifuatilia elimu iliyotolewa na Wizara ya Fedha, pamoja na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), TCB, NMB, CRDB na NBC, yaliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Busekera, mkoani Mara.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WF, Mara)
Na. Josephine Majura WF, Mara.
Wizara ya Fedha inaendelea na zoezi la utoaji elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi yote ikiwa ni utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa mwaka 2021/2022 hadi 2029/2930.
Hadi sasa Wizara ya Fedha imetoa elimu ya fedha katika mikoa 15, ikiwemo mkoa wa Kagera, Singida, Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Kigoma, Pwani, Morogoro, Rukwa, Lindi, Mtwara, Tabora, Shinyanga, Simiyu na Mara.
Katika zoezi la utoaji elimu ya fedha Wizara ya Fedha, imeambatana na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, NSSF pamoja na Taasisi za Benki ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), TCB, NMB, CRDB na NBC.
Post A Comment: