Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Benki ya Access ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Bw. Protase Ishengoma, baada ya kufanya ziara fupi ya kutambulisha shughuli za Benki hiyo, katika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam,  na kujadiliana kuhusu fursa za ushirikiano kati yake na Serikali katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.


Katika Kikao hicho kilihohudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha ambaye pia ni Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Benki hiyo, Mhe. Dkt. Nchemba, alitoa wito kwa Taasisi za Fedha nchini, kuiwezesha sekta binafsi kupata mitaji ili iweze kuchangia kwa kiwango kikubwa ukuaji wa Uchumi, kukuza ajira na maendeleo ya nchi kwa ujumla.


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Access Bank, Bw. Protase Ishengoma, aliipongeza Serikali kwa kutekeleza miradi mikubwa ya kijamii ikiwemo ile ya kimkakati na kuahidi kuwa Benki yake ambayo ina misuli ya kifedha, iko tayari kushiriki katika ujenzi wa miradi mbalimbali nchini ikiwemo pia kuwa miongoni mwa Taasisi zinazoweza kufanya majukumu ya kuitafutia Serikali fedha za kutekeleza miradi hiyo.

Share To:

Post A Comment: