Na. Peter Haule, WF, Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Afritac East, iliyoko chini ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Clara Mira, kuhusu program ya kuongeza ujuzi na kuangalia maeneo mahususi ya kuongeza uwezo.
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) linaendesha program ya kuongeza ujuzi katika baadhi ya nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania, Rwanda, Uganda, Kenya, Eritri na Malawi.
Mkutano huo ulihudhuliwa pia na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw. Sebastian Acevedo na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera, Wizara ya Fedha, Dkt. Remidius Ruhinduka.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akiagana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Afritac East iliyoko chini ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Clara Mira, baada ya mazungumzo yao kuhusu program ya kuongeza ujuzi na kuangalia maeneo mahususi ya kuongeza uwezo, mazungumzo yaliyofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akiteta jambo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Afritac East iliyoko chini ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Clara Mira, baada ya mkutano wao kuhusu program ya kuongeza ujuzi na kuangalia maeneo mahususi ya kuongeza uwezo, mazungumzo yaliyofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akiongoza mkutano kati yake na Mkurugenzi wa Taasisi ya Afritac East iliyochini ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Clara Mira (wa pili kushoto), ambapo walijadili kuhusu program ya kuongeza ujuzi na kuangalia maeneo mahususi ya kuongeza uwezo, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw. Sebastian Acevedo, akieleza kuhusu program ya kuongeza ujuzi kwa nchi nane za Afrika ikiwemo Tanzania, wakati wa mkutano kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, (kulia) na Mkurugenzi wa Taasisi ya Afritac East iliyochini ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Clara Mira (hayupo pichani), uliofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.

Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera, Wizara ya Fedha, Dkt. Remidius Ruhinduka, akieleza umuhimu wa kuongeza ujuzi kwa watanzania wakati wa mkutano kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, (kulia) na Mkurugenzi wa Taasisi ya Afritac East iliyochini ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Clara Mira (hayupo pichani), uliofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mchumi kutoka Idara hiyo, Bi. Neema Mtei.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akisikiliza maelezo ya Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw. Sebastian Acevedo (kushoto), kuhusu program ya kuongeza ujuzi kwa nchi za Afrika ikiwemo Tanzania, wakati wa mkutano kati yake na Mkurugenzi wa Taasisi ya Afritac East iliyochini ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Clara Mira (kulia), uliofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Afritac East iliyoko chini ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Clara Mira (wa tatu kushoto), Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw. Sebastian Acevedo (wa pili kulia), na wajumbe wengine kutoka Wizara ya Fedha na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), baada ya mkutano wao kuhusu program ya kuongeza ujuzi kwa watanzania Tanzania, uliofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Dar es Salaam)
Post A Comment: