Na. Saidina Msangi, WF, Dodoma

Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine, kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu – El Maamry Mwamba, amefanya mazungumzo na ujumbe kutoka Danish Public Investment Fund for Development Countries (IFU), ukiongozwa na Balozi wa Denmark Nchini, Mhe. Jepser Kammersgaar, katika Ofisi za Wizara ya Fedha, jijini Dodoma.

Mazungumzo yao yalilenga kujadili fursa mbalimbali zikiwepo za mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta za maji na nishati. 

Aidha, kupitia Mfuko huo Tanzania inaweza kunufaika na aina mbalimbali za ufadhili unaotolewa na Mfuko huo ikiwemo uwekezaji wa hisa (equity investment), na dhamana (guarantees).

Kikao hicho kilihudhuriwa na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Mfuko wa IFU, anayeshughulikia Sekta ya Umma katika Mikopo Nafuu na Misaada, Bi. Tina Kollerup Hansen, na Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Dhamana, Bw. Theo Ib Larsen.

Kwa upande wa Wizara ya Fedha kikao hicho kilihudhuriwa na Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Bw. Melckzedeck Mbise na Kamishna Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali, Bi. Tiba Kisonga.

Share To:

Post A Comment: