MKUU wa Wilaya ya Rombo, Raymond Mwangwala, amesema kuwa endapo wananchi wataelewa umuhimu kulipa kodi na athari za biashara za magendo nchi itakuwa salama.

Hayo ameyasema hivi karibuni wakati wa ziara ya Maofisa wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) , idara ya forodha.

DC. Mwangwala amesema kuwa amewapa baraka maofisa hao kwenda kuwapa elimu wananchi.

"Elimu ni muhimu hatuzungumzii tu magendo , tunazungumzia mtu anaweza kuingiza silaha , mtu anaweza kuingia sumu ambayo itaathiti nchi yetu mtu anaweza wahamiaji harama ambao huwezi kuelewa ni maharamia au magaidi kwa hiyo tunapozungumzia kuangalia mipaka yetu hatuzungumzi kwenye muktadha wa kodi tu , tunazungumzia muktadha wa kiusalama, mapato , tunazungumzia mambo ambayo mwananchi akiyaelewa utakuwa msaada mkubwa kwa nchi yetu".

"Nendeni mtusaidie elimisheni watu waweze kuelewa tunakuwa tumeisaidia nchi yetu kwa kiasi kikubwa" .

Amependekeza kuwa elimu hiyo itolewe kwa Watendaji na wenyeviti wa vitongoji ambao hawa wako karibu na wananchi.

Amesema kuwa endapo mapato yakakusanywa vizuri basi nchi itapata maendeleo.

"Mnafanya hivyo lengo letu kuisaidia nchi , tunakuwa tuwasaidia Watanzania na tunakuwa tumemsaidia Rais wetu "

Amesema kuwa endapo wananchi wakaelewa umuhimu wa kodi na usimamizi ukawa nzuri basi nchi itajisimamia .

"Hakuna mtu atakayeweza kutunyanyasa kwa sababu tunakuwa na uwezo wa kujiendesha wenyewe ...mapato ya ndani tunaambiwa sasa yanafikia asilimia 70 kwa hiyo kama tumefika hatua hiyo tunaweza kujiendesha wenyewe".

Ametoa wito kwa maofisa wa TRA kufanya shughuli zao kwa uadilifu.

Ameitaja changamoto ya maeneo ya mipaka kutorasimishwa kwenye forodha kwa kuwa kuna njia zinazotumika kutoka ambapo haziwa mawakala wa forodha.
Share To:

Post A Comment: