Katibu tawala mkoa wa Kagera bi.Proscovia Mwambi amesema bukoba imejipanga kuwa mfano wa kuigwa katika usalama wa chakula kwa maana ya (Safety kwenye Masoko).

Bi.Mwambi alisema kuwa kwa kuwa mkoa huo ni mzuri kwenye uzalishaji basi jitahidi zinatakiwa kuongezeka katika eneo hilo la Usalama wa Chakula.

Ameyasema hayo leo alipofungua semina kuhusu Usalama wa Chakula "Food Safety "iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Agri Thamani kwa kushirikiana na shirika la  kimataifa la Global Alliance for Improved Nutrition (GAIN).

 Katibu tawala huyo alisema kuwa kwa kuwa wadau muhimu wameshirikishwa basi ni wazi kuwa mkoa wake utafanya vema na yeye kama msimamizi atahakikisha kuwa anasimamia jambo hilo na kuwa kinara katika eneo hilo la Usalama wa Chakula.

Semina hiyo imekutanisha washiriki 180 kutoka bukoba mjini ambao ni viongozi wa soko la kashai, Rwamishenye,Custom,Nyakanyasi,na Soko kuu.

Mkurugenzi wa Shirika la Agri Thamani  bi.Neema Lugangira amesema wameamua kushirikiana na GAIN ili kuhakikisha kuwa wadau hao wanapata uelewa wa usalama wa chakula kwa kuwa ni wafanyabiashara wa maeneo yao na wataweza kuboresha shughuli zao.

Aidha alisema pia wadau wengine walioshiriki ni pamoja na wauza mboga mboga,samaki,matunda wa masoko hayo,viongozi wa serikali za mitaa na.kata mbali mbali bila kusahau maafisa kutoka manispaa ambao ni kutoka vitengo vya lishe,afya,kilimo na mifugo.

"Hawa ni wadau muhimu ambapo tumeona tushirikiane nao katika kuhakikisha kuwa uhifadhi wa chakula unazingatia usalama na walaji hawaathiriki na uelewa huu wengi hawana,hivyo kuwezesha jamii kuweza  kuhifadhi chakula katika mazingira mazuri."Alisisitiza Mkurugenzi huyo.













Share To:

Post A Comment: