Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa leo tarehe 16 Machi, 2025 amewasili Mkoa wa Geita ambapo amepokelewa na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa Geita Martine Shigela na Viongozi wengine wa Mkoa huo.

Bashungwa akiwa Mkoa wa Geita anatarajia kuungana Wananchi na Waumini kushiriki Ibada ya Misa ya kumuombea Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli inayotarajiwa kufanyika kesho tarehe 17 Machi 2025 Wilayani Chato.
Share To:

Post A Comment: