Wizara ya Maliaisili na Utalii imetakiwa kubuni mazao mapya ya Utalii ambao unawezekana kufanyika katika eneo la Mapango ya Amboni yaliyopo katika Jiji la Tanga ili kuongeza idadi ya watalii katika eneo hilo na Hifadhi ya Mikoko ya Sahare

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Timotheo Mnzava (Mb) wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa lango la kuingilia katika eneo la Mapango.

Mhe. Mnzava aliongeza kuwa uboreshaji wa Lango la kuingia katika eneo Hilo uendane na kuongeza mazao mengine ya Utalii katika eneo Hilo.

“Naitaka Wizara itakapokuja Bungeni ituletee mpango mkakati wa kuongeza mazao ya Utalii katika eneo hili,hapa Tanga karibu na Unguja na Pemba na maeneo yale yanasifika kwa kuwa na vivutio vya Utalii, tunataka watalii wale wakitoka Zanzibar waje Tanga kisha waende kwenye maeneo Mengine” Alisema Mhe. Mnzava.

Kamati ipo katika Jiji la Tanga ambapo imetembelea Mradi wa ujenzi wa Lango la kuingilia katika Mapango ya Amboni na Hifadhi ya Mikoko ambapo katika eneo Hilo Kuna Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Utalii ikiwa na Lengo la kukagua maendeleo ya miradi ya maendeleo inayofanyika katika wizara ya maliasili na Utalii.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameishukuru kamati kwa kutembelea Miradi hiyo na Yale yote yaliyoshauriwa yataendankufanyiwa kazi.

“Kamati imetushauri mambo mengi lakini kubwa ni kuongeza mazao ya Utalii katika Jiji letu la Tanga kama zip lining, campsite katika eneo la Amboni” alisema Mhe. Chana lakini utalii wa kutembelea msitu wa Mikoko katika eneo la Sahare”

Mhe. Chana alitumia fursa hiyo kuwaomba wawekezaji kuwekeza katika hifadhi za misitu kama ambavyo wanavyowekeza katika hifadhi za Wanyama.     

Share To:

Post A Comment: