Wananchi hao wametoa ombi hilo wakiwa kwenye mkutano wa kampeni ya msaada wa kisheria ulioandaliwa na timu ya msaada wa kisheria kwa lengo la kutoa elimu, kusikiliza na kutatua migororo mbalimbali ya wananchi katika kijiji hicho. Katika ombili hilo wananchi wamependekeza zoezi hilo lifanyike kila baada ya kipindi cha miezi sita hadi mwaka mmoja ili kuendelea kuwapatia fursa wananchi kupata uelewa na msaada ya masuala ya kisheria ambayo kwa kiasi kikubwa wamesema hawana uelewa nayo na hali ambayo inasababisha kukosa haki zao pamoja kutokea kwa migogoro ya mara kwa katika jamii yao.
Aidha katika kijijiji hicho wa timu ya kampeni ya msaada wa kisheria imefanikiwa imesikiliza, kutatua na kutoa ushauri wa kisheria migogoro zaidi ya 100 ambayo 60 kati hiyo ni migogoro inahusu masuala ya ardhi. Akijibu ombi la wananchi hao mratibu wa kampeni ya msaada wa kisheria wilaya ya Liwale Wakili Abdul Bwanga amesema kupitia kampeni hiyo katika halmashauri ya wilaya ya Liwale tayari serikali imeandaa maafisa msaada wa kisheria ambao watakuwa wanatoa huduma muda wowote kwa wananchi watakaohitaji huduma.
Zoezi hilokampeni ya msaada wa kisheria kwa sasa linaloendelea kwa muda wa siku tisa katika wailaya ya Liwale ambapo lilianza tarehe 19 Februari na linatarajiwa kutamatika tarehe 28, Februari mwaka.
Post A Comment: