Mkakati wa Uchumi wa Kidijitali hapa nchini Tanzania utekelezwaji wake unatarajiwa kukamilika Octoba mwakani na hivyo huduma za kidijitali zinatarajiwa kutumika kila mahali na kwa watu wote nchini.
Akizungumza na Wanahabari mkoani Arusha mkurugenzi wa Mifumo na teknolijia ya habari Mohamed Mashaka kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya habari amesena mradi wa Tanzania ya Kidijital ulianza utekelezaji wake Mwaka 2021 na unatarajiwa kukamilika 2026 Oktoba.
" Huu ni mradi wa Miaka mitano ambao ulianza tangu 2021 na unakamilika mwakani mnamo mwezi wa 10 na faida moja wapo kwa mradi huu ni kutoa huduma bora kwa wananchi na kwa wakati na ni mradi mkubwa kwa nchi" amesema.
Amesema kwa sasa umefikia asilimia 80 tangu walipoanzisha na lengo la kikao kinachoendelea mkoani Arusha ni pamoja na kufanya tathmini ya mradi huo ambao wabia wa mradi ni pamoja na benk kuu ya dunia.
Priscus Tairo ni Mkurugenzi msaidizi wa Utumishi wa uma kutoka ofisi ya Rais ambapo amesema kuwa mradi huo umewawezesha katika usimamizi wa utendaji kazi wa watumishi wa uma na taasisi zote za uma ambapo ameomgeza kuwa hivi karibuni wanampango wa kuanzisha daftari la huduma za wateja lenge ikiwa ni kuwezesha wananchi kupata huduma za pamoja.
Naye mkurugenzi wa usimamizi wa Mifumo ya tehama NIDA Con Frances amesema mfumo huo umetumika katika kuwezesha kupatikana namba ya Utambuzi kwa watu wote kupitia NIDA hivyo ni msaada mkubwa na wanaendelea kutekeleza agizo la Rais wa Tanzania La kuwepo kwa namba moja ya Utambuzi wa wananchi wote.
"Kupitia mradi huu NIDA imeweza kusaidiwa kuanza kufanya taratibu za kubadilisha sheria kwa sababu katika hawa watu milioni 25 ambao tayari wameshasajiliwa NIDA watu wazima ni kuanzia miaka 18 kwenda juu lakini miaka 17 hawakutambuliwa na NIDA hivyo utaratibu wa kutambua ni teknolojia nyingine lakini tunaamini kupitia mradi huu tutapata uwezo wa teknolojia rahisi ya Kuwatambua watoto" amesema.
Post A Comment: