![](https://lh3.googleusercontent.com/-9bVMfnUZpTg/Z64OnycbR2I/AAAAAAAB-DY/P3g0JKSU0iEzak9ItVydtoRD27iWI9crgCNcBGAsYHQ/s1600-rw/1001111993.jpg)
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imefanya mafunzo kwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za Serikali(PAC) na Sheria Ndogo juu ya uendeshaji wa Mamlaka katika majukumu yake ya Ki udhibiti na Uongozaji ndege.
Pia utekelezaji wa miradi mbalimbali yenye lengo la kuendelea kuliweka anga la Tanzania salama. Semina hiyo imefanyika Februari 13, 2025 Bungeni Jijini Dodoma
Lengo la semina hiyo ni kuwajengea uelewa wa pamoja waheshimiwa wabunge kuhusu Mamlaka na namna inavyotekeleza viwango vya kimataifa kwa mujibu wa taratibu za Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO).
Katika semina hiyo Kamati hizo ziliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Hesabu za Serikali(PAC) Mhe Japhet Hasunga kwa niaba ya wenyekiti wa Kamati zote mbili ambapo Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa anga Tanzania (TCAA) Bw.Salim Msangi akiambatana na wataalamu wake walitoa ufafanuzi kuhusu mambo mbalimbali kufuatilia maswali ya waheshimiwa wabunge.
![](https://lh3.googleusercontent.com/-PjbjQ5nO_6E/Z64OoeNy_pI/AAAAAAAB-Dc/_9IiG6-EpekMdX1wSCac3s7pcpxg0srSACNcBGAsYHQ/s1600-rw/1001112007.jpg)
Mhe. Hasunga amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada anazofanya kwa kutenga fedha zaidi za kutekeleza miradi ya mamlaka ikiwemo Ujenzi wa Chuo cha kisasa cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC,) mradi ambao hadi kukamilika kwake utagharimu shilingi bil 78. Pia amempongeza Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David kihenzile aliyekuwepo kwa niaba ya Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa kwa kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na kupatikana kwa fedha za kutekeleza miradi hiyo.
“Leo tumepata mafunzo ya muhimu sana hasa namna Mamlaka inavyosimamia shughuli mbalimbali zinazokuwa zikiendelea kwa watoa huduma mbalimbali, sisi kama Kamati za Bunge tunasimamia na kuangalia namna taasisi zetu za umma zinavyotekelea majukumu yake tumejifunza namna marubani wanavyorusha ndege, mawasiliano baina ya muongozo ndege na rubani yanavyofanyika kwa usalama na tumeridhika" amesema Mje. Hasunga
Aidha, akifunga mafunzo hayo Mhe. Hasunga ameiomba Serikali kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kukamilisha miradi ya Mamalaka inayoendelea ili kuzidi kuboresha usalama wa anga letu na kuendelea kuvutia jumuiya za kimataifa
![](https://lh3.googleusercontent.com/-PInTkrRVvbc/Z64Oo8jwboI/AAAAAAAB-Dg/jwRF8UaNRrQtwJ01sckoGQStd_L4cwWVwCNcBGAsYHQ/s1600-rw/1001112006.jpg)
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile amewashukuru wabunge wa kamati zote mbili kwa kutenga mda wao na kupata mafunzo kupitia semina hiyo licha ya kuwa na ratiba ngumu za shughuli za Bunge zinazoendelea na kuahidi Wizara na taasisi zake zitaendelea kushirikiana na kamati zote.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa anga Tanzania Salim Msangi alitoa taarifa za miradi, mikakati na shughuli mbalimbali za maendeleo zinazotekelezwa na Mamlaka ambazo zinachangia anga la Tanzania kuwa salama kitaifa na kimataifa.
![](https://lh3.googleusercontent.com/-FN6OAHk7bkY/Z64OpQaqkBI/AAAAAAAB-Dk/nGtSm2HW8Y0ZMY85G3jkLCeKbbg9n947wCNcBGAsYHQ/s1600-rw/1001111996.jpg)
![](https://lh3.googleusercontent.com/-Bfv7zLBLnkY/Z64Op0m4kaI/AAAAAAAB-Do/dQzTkiOrvaArxEQkm-S0OeEzKExVNr9IwCNcBGAsYHQ/s1600-rw/1001111999.jpg)
![](https://lh3.googleusercontent.com/-225XJdcR8aw/Z64OqY_RpiI/AAAAAAAB-Ds/YC_OPOjc9wg9H7Tta3fld0qMnaWbW1l-wCNcBGAsYHQ/s1600-rw/1001112020.jpg)
![](https://lh3.googleusercontent.com/-q-wxSS-n75c/Z64Oq4mErGI/AAAAAAAB-Dw/f_vNQN3nYv0fv9WDNcH-0l9ggKPlyjjzQCNcBGAsYHQ/s1600-rw/1001112023.jpg)
![](https://lh3.googleusercontent.com/-oIfdzh4nZKI/Z64OrkmyRgI/AAAAAAAB-D0/QqdFhqGFzR4CYHWSf4yCzzgbWakSTPDNwCNcBGAsYHQ/s1600-rw/1001112011.jpg)
![](https://lh3.googleusercontent.com/-y2PuWt4M3k8/Z64Or3QmDXI/AAAAAAAB-D4/Ybpx9myB4PITn2yQcl5dR8ON6b_zeGU5QCNcBGAsYHQ/s1600-rw/1001112015.jpg)
![](https://lh3.googleusercontent.com/-SwWxaQ4lPdU/Z64OsZQQ80I/AAAAAAAB-D8/owGai6ifj0A9c-IkCl8sMx1jxRjD_FAAgCNcBGAsYHQ/s1600-rw/1001111987.jpg)
![](https://lh3.googleusercontent.com/-g9fb5VVkkac/Z64Os31_MbI/AAAAAAAB-EA/79446dlf1O0uR6b4iB-a_BzB9kGlAvLUQCNcBGAsYHQ/s1600-rw/1001111995.jpg)
Post A Comment: