Naibu Waziri Nishati,  Mhe. Judith Kapinga amesema kuwa Serikali imeboresha mazingira ya wanawake nchini ili waweze kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za kiuchumi, maendeleo ya Tanzania na kushika nafasi za uongozi.

Mhe. Kapinga ameyasema hayo alipokuwa akielezea nafasi ya mwanamke katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya  Wanawake Duniani ambayo nchini yatafanyika mkoani Arusha.

"Kipekee namshukuru na kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani amekuwa dira ya kutuongoza na kuhakikisha wanawake wengi zaidi tunashiriki katika shughuli za maendeleo na hata katika nafasi za uongozi." Amesema Mhe. Kapinga

Amesema Rais Samia amekuwa kinara katika kuibua wanawake katika sekta mbalimbali za kiuchumi nchini. 

Ameitaka jamii kuondokana na dhana kwamba mwanamke anapopewa nafasi ya uongozi anaweza kusahau majukumu yake mengine ya kijamii.

 Aidha, Mhe. Kapinga ametoa wito kwa wanawake kupendana, kushikamana, kusaidiana na kutembea kifua mbele katika kuelekea Siku ya Wanawake  Duniani.

Share To:

Post A Comment: