Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwan Kikwete, Mapema leo Jumatatu Februari 17, 2025 Jijini Arusha, amekutana na kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda akimpongeza kwa uchapakazi na utendaji wake katika kuwahudumia wakazi wa Mkoa huo tangu kuteuliwa kwake kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika Leo Jumatatu Februari 17, 2025, Mhe. Makonda kando ya mengineyo, amemueleza Mhe. Kikwete kuhusu maandalizi yanayoendelea Jijini Arusha, wakati huu Mkoa wa Arusha ukijiandaa kuwa Mwenyeji wa Wiki ya wanawake duniani yanayotarajiwa kufanyika kuanzia Machi 01- 08, 2025, Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Tumejipanga vizuri kuelekea  maadhimisho haya na tunategemea kuwa na Wizara 10 ikiwemo Wizara ya Katiba na sheria na Samia Legal Aids watakuwepo kwaajili ya kutatua kero na changamoto zote za wananchi wa Mkoa wa Arusha." Amesema Mhe. Makonda.

Mhe. Kikwete ameambatana na kamati ya kudumu ya Bunge ya  Ustawi na Maendeleo ya jamii ambao wamepangiwa kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kutembelea eneo la Mradi mkubwa wa ujenzi wa Ukumbi wa Mikutano utakaokuwa na uwezo wa kuhudumia zaidi ya watu 4000 kwa wakati Mmoja kwenye eneo la Impala pamoja na kukagua kampeni ya mfuko wa jamii NSSF ya kusajili wananchi wenye kipato kidogo kwenye mfumo mpya wa Pensheni kupitia maadhimisho ya Wiki ya wanawake inayotarajiwa kufanyika Mkoani Arusha na kufikia kilele chake Machi 08, 2025.








Share To:

Post A Comment: