Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Ijumaa Februari 28, 2025, anaendelea na ziara yake Mkoani Tanga kwenye Jimbo la Tanga Mjini, akitarajiwa kuwa na mkutano mkubwa wa hadhara wa kuzungumza na wananchi kwenye viwanja vya Mkwakwani Jijini Tanga.

Aidha kulingana na ratiba iliyotolewa awali na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Batilda Buriani, Rais Samia akiwa Jijini Tanga Kesho Jumamosi Machi 01, 2025 atatembea na kukagua maboresho makubwa ya bandari ya Tanga ambapo takribani Bilioni 429 zimetolewa kuboresha bandari hiyo kwa kuongeza kina chake ili kuruhusu kutia nanga kwa meli kubwa.


Awali katika ziara yake Mkoani Tanga, Rais Samia akiwa Handeni alizindua Hospitali ya wilaya hiyo, Kuzindua jengo la Halmashauri ya Lushoto, kuzindua mradi wa maji Mkomazi, Uzinduzi wa barabara ya Tanga - Pangani -Saadan -Bagamoyo, Kuzindua shule ya sekondari ya sayansi kwa Wasichana ya Beatrice Shelukindo pamoja na kuzindua mradi wa maji Mkinga.


Rais Samia pia aliweka jiwe la msingi la upanuzi wa msikiti mkuu wa Ijumaa Pangani pamoja na Februari 27, 2025 kuwa Mgeni Rasmi kwenye Uwekaji wa Jiwe la msingi la upanuzi wa Ujenzi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa, Tanga Mjini.

Share To:

Post A Comment: