Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, anayeshughulikia Elimu, Dkt. Charles Mahera, amekutana na Mbunge wa Bunge la Ulaya, Gyorgy Holvenyi, pamoja na Andras Szenczi, mshauri wa maendeleo katika Bunge hilo kujadili utekelezaji wa fedha za GPE nchini (Global Partnership for Education)

Kikao hicho kilichofanyika Jijini Dar es Salaam Februari 25, 2025 kiliudhuriwa na Wadau wa Maendeleo, Martha Makala Mkurugenzi Mtendaji TENMET (Tanzania Network for Education and Micro-Enterprise Technology)

 Stella Mayenje Meneja Mkuu wa Programu GPE Ubalozi wa Uswidi nchini na Lydia Wilbard Mkurugenzi Mtendaji CAMFED (Campaign for Female Education) kimejadili namna Mradi huo unavyoongeza ujumuishi wa fursa za kupata elimu kwa watoto wa kitanzania.

Tanzania ni moja ya nchi zinazonufaika na ufadhili kutoka GPE na sasa umelenga katika kuleta mabadiliko ya kimfumo katika sekta ya elimu nchini kwa kuboresha kada ya ualimu kama chachu ya matokeo chanya ya ufaulu wa mwanafunzi.
Share To:

Post A Comment: