Naibu Katibu Mkuu, Bw. Ismail Rumatila pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt.Grace Magembe wameongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa Bodi Tendaji ya 156 ya Shirika la Afya Duniani unaofanyika kuanzia leo Feberuari 3 hadi 11, 2025 Geneva-Uswisi.
Mkutano huo unalenga kujadili ajenda mbalimbali zitakazowasilishwa wakati wa Mkutano wa 78 wa Shirika la Afya Duniani utakaofanyika mwezi Mei 2025.
Wakishiriki katika vikao vya awali, Naibu Katibu Mkuu ameshiriki kikao cha pembezoni cha kujadili Mikakati ya kujumuisha Afya ya mtu binafsi katika Afya kwa wote iliyoandaliwa na Global Self Care Federation na the United -Self Care Coalition.
Aidha, Mganga Mkuu wa Serikali ameshiriki katika vikao vya awali vya Kikundi Kazi cha Afrika kwa ajili ya kuweka maandalizi ya uwasilishaji kabla ya kikao cha Mkutano wa Bodi Tendaji kuanza.
Post A Comment: