Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo amewaagiza wataalamu kutoka Wizara yake kufanya tathmini kuhusu kujenga uwanja wa mazoezi kwaajili ya mashindano ya AFCON katika eneo la FFU, Morombo Jijini Arusha.

Naibu Waziri Mwinjuma ametoa maagizo hayo leo tarehe 15 Februari, 2025 wakati akizindua michuano ya Soka ya Chuga Cup 2025 baada ya ombi la Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mhe. Mrisho Gambo kuomba eneo hilo ujengwe uwanja wa kisasa kwaajili ya mazoezi wakati wa michuano ya Kombe la Mataifa Barani Afrika AFCON 2027 ambayo Tanzania ni miongoni mwa nchi mwenyeji.

Aidha, Mhe.Mwinjuma amesema wananchi wa Arusha wanayo kila sababu ya kuendelea kumwamini Mbunge wao Gambo kwa sababu amekuwa akipigania miradi mbalimbali ya wananchi Jijini humo ikiwemo wazo la kujenga uwanja wa kisasa wa mpira wa Miguu Jijini humo tangu akiwa Mkuu wa Mkoa.































Share To:

Post A Comment: