Na Oscar Assenga, Tanga

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Jacobs Mwambegele amesema kwamba mawakala, viongozi wa vyama vya siasa hawapaswi kuingilia mchakato wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura vituoni.

Mchakato wa zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura likitarajiwa kuanza mkoani Tanga February 13 mwaka huu imeelezwa kwamba

Jaji Mwambegele aliyasema hayo leo wakati akifungua mkutano wa Tume na wadau wa Uchaguzi Mkoani Tanga ambapo alisema ni lazima viongozi wa vyama hivyo na wadau wa uchaguzi kuzingatia sheria ya uchaguzi.

Alisema pia wazingatie kanuni za uboreshaji, maelekezo ya Tume na kusimamia miiko na mipaka ya uendeshaji wa zoezi la uboreshaji wa daftari .

Aidha alisema iwapo kutatokea changamoto wakati wa zoezi la uboreshaji ni vyema wakatumia taratibu zilizoainishwa katika sheria zinazosimamia uchaguzi ikiwemo kuziwasilisha changamoto hizo katika tume hiyo kwa ajili ya kuzipatia ufumbuzi.

Katika hatua nyengine Mwenyekiti huyo wa Tume alisema watakaobainika kujiandikisha zaidi ya mara moja watakuwa wametenda kosa la jinai na adhabu yake inaweza kuwa kifungo kwa kipindi kisichopungua miezi sita.

Alisema pia kwamba watakumbana na kifungo kisichozidi miaka miwili gerezani au vyote pamoja ikiwemo faini ya moja na usiozidi laki tatu.

Jaji Jacobs aliwaasa wananchi kujiepusha na kosa la kujiandikisha zaidi ya mara moja ili kuepuka uvunjaji wa sheria kutokana na kufanya hivyo ni kosa la jinai kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 114(1) cha sheria ya uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani namba ya mwaka 2024.

“Nitumie fursa hii kuwaasa wananchi wa mkoa wa Tanga kujiepusha na kosa la kujiandikisha zaidi ya mara moja na niwaombe wadau mliopo hapa mkawaelimishe wananchi kwamba wakajiandikishe mara moja na kwenye kituo kimoja ili kuepuka uvunjaji wa sheria”Alisema

Aidha alisema kwamba zoezi hilo la uboreshaji wa daftari haliwahusu wapiga kura wenye kadi ambazo hazijaharibika au kupotea au hawajahama kutoka eneo moja la uchaguzi kwenda eneo jingine au taarifa za hazijakosewa au hawahitaji kuboresha taarifa zao.

“Lakini pia tume imeweka utaratibu kwa watu wenye ulemavu, wazee, wagonjwa, wajawazito na wakina mama wenye watoto wach anga watakaokwenda nao vituoni kupewa fursa ya kuwahudumia bila kupanga foleni”Alisema

“Hivyo tunawaomba wadau wa uchaguzi muwafahamishe wananchi wote waliopo kwenye makundi tajwa kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha au kuboresha taarifa zao vituoni kwa kuwa utaratibu mzuri wa kuwahudumia umewekwa”Alisema
Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: