Kaimu katibu tawala wa Mkoa wa Lindi Natalis Linuma akizungumza na wataalamu mbili mbali katika kikao kazi cha mafunzo kuelekea kwenye uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia legal Aid kikao kilichokufanya Ruangwa wilayani lindi na kuhudhuriwa na wataalamu kutoka katika Halmashauri zote za Mkoa wa Lindi
Wataalamu mbili mbali katika kikao kazi cha mafunzo kuelekea kwenye uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia legal Aid kikao kilichokufanya Ruangwa wilayani lindi na kuhudhuriwa na wataalamu kutoka katika Halmashauri zote za Mkoa wa Lindi
Wataalamu mbili mbali katika kikao kazi cha mafunzo kuelekea kwenye uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia legal Aid kikao kilichokufanya Ruangwa wilayani lindi na kuhudhuriwa na wataalamu kutoka katika Halmashauri zote za Mkoa wa Lindi


Mama Samia legal Aid yafanya mafunzo ya kikao kazi cha usaidizi kwa wataalamu na watakao shiriki katika kutoa huduma ya msaada wa kisheria kutoka wilaya zote za Mkoa wa Lindi ambapo kesho ufunguzi rasmi wa kampeni  katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi Na kufunguliwa na Waziri Mkuu wa jamuhuri ya Tanzania.


Tayari mikoa 17 ya Tanzania bara tayari imesha fanyaka uzinduzi wa kampeni na Leo tarehe 18 Februari usinduzi unafanyika katika Mkoa wa Mwanza n lengo Hadi kufikia mwisho wa mwezi huu iwetayari wamesha fikia mikoa 22.


Natalis Linuma kwa niaba ya katibu tawala wa Mkoa wa Lindi Amesema mafunzo hayo ya kikao kazi Amesema anamshukuru sana Rais Samia kwa kutoa kuweza kutoa malekezo kwa wizaran ya katiba na sheria kwakuhakikisha kunakua na program ya kutoa elimu kwa wanainchi kwa kuweza kupata msaada wa kisheria katika kutatua changamoto mbali mbali za kisheria.


Aitha Linuma ametoa wito kwa wataalamu hao waweze kuelewa namna ya kuweza kuwasaidia na  kuwaelewesha wanainchi kwenye maeneo watakayo kwendaa.kwasababu wanainchi hao wanahitaji haki za binaadam na utawala Bora.


Pia Linuma amewataka wataalamu mufunzo hayo yakawe chachu na mwangaza Ili kwenda kupunguza migogoro kwenye maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Lindi.


"Kwa hawa ambao wanapata mafunzo leo waweze kujifunza na kuelewa jinsi ya kuwaelewesha na kuwasaidia wanainchi kule wanakoenda Mkoa wetu wa Lindi ni miongoni mwa mikoa ambayo tunazo changamoto za kawaida na kisheria katika sehemu mbali mbali, kuhusu migogoro ya ardhi, Migogoro ya mirathi pamoja na maswala ya ndoa."


Nae Ester Msambazi Mkurugenzi huduma za msaada wa kisheria wizaran ya katiba na sheria Amesema kwa kushirikiana na wadau wanatekeleza kampeni yenyejina la mama Samia legal Aid kampeni ambayo inatekelezwa katka ngazi ya kijiji n jamii kwa lengo kuwafikia wanainchi walio maeneo ya pembezoni ambao hawapati huduma za kisheria.


Aitha Ester Msambazi Amesema kampeni imetokana na ombwe kubwa kwakua wanainchi wengi hawana uelewa juu ya msaada wa kisheria hata wanapokua wamepata changamoto wanakua hawajui wapi kwa kukimbilia na kutatua changamoto zao.


"Lengo la kwanza kabisaa tunataka wanainchi wapate  uelewa kuhusuana na masuala ya kisheria na upatikanaji wa haki za kwa wanainchi kwa kupitia huduma za msaada wa kisheria mwanainchi yeyote ambae anahitaji msaada wa kisheria na anashindwa kwenda mahakamani kwasababutu hana muwakilishi Wala wakili basi atapata huduma hizo kwa kupitia msaada wa kisheria"Amesema Ester Msambazi 


Andrew Munisi afisa aridhi mteule manispaa ya Lindi amesema kampeni hizo za msaada wa huduma za kisheria ya mama Samia itaenda kuondoa changamoto za kisheria pamoja na kutoa elimu kwa wananchi.



"Tunamatarajiao makubwa kama idara ya aridhi kunachangamoto nyingi sana kama migogoro ya wakulima na wafugaji,migogoro ya kifamilia kama watu wa aridhi tunamatarajiao ya kutoa msaada wa kisheria sekta ya aridhi"amesema Munisi


Munisi ameongeza kwakusema kwakiasi kikubwa wanaenda kutatua hizo changamoto watakapoenda kutoa msaada wakisheria.


"Kwakiasi kikubwa tunaenda kutatua hizo changamoto tutakapotoa msaada wakisheria wananchi wataelewa nini chakufanya lakini kama kunamtu anataka ushauri wakisheria hivyo itamsaidia kuondoa hizo changamoto.Hii kampeni itaenda kuleta usawa,utulivu,haki  na maendeleo"amesema Munisi.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: