Mapitio na uhuishaji wa mitaala ni muhimu katika kuifanya iwe ya kisasa zaidi kwa kuangalia kinachohitajika katika soko la ajira, ili kumfanya mwanafunzi aweze kujiajiri na kuajiriwa baada ya kuhitimu.
Hayo yameelezwa na Dkt. Grace Idinga, Naibmkuu wa Chuo taaluma, utafiti na ushauri wa kitaalam wakati wa kikao maalum cha mapitio ya mitaala chini ya mradi wa heet, kilichofanyika Februari 11 na 12, 2025 katika ukumbi wa Intel, Arusha
Dkt. Grace amesema kuwa Chuo Cha Uhasibu Arusha kwa kiasi kikubwa kimefanikiwa katika kuandaa na kupitia mitaala chini ya mradi wa heet, ambao mitaala 8 iliyo ndani ya mradi huo inaboreshwa kwa kuzingatia utaratibu wa kuangalia maoni ya wanafunzi
Akizungumza katika kikao hicho, Joramu Nkumbi mwenyekiti wa kamati ya heet amesema kuwa, kikao hicho ni muhimu sana katika kushauri chuo kuhusu yale ya kuwafunza wanafunzi hususani mafunzo kwa vitendo, ili kuwawezesha wanafunzi kukabiliana na ushindani kwenye soko la ajira
Kwa upande wake Catholic Sumuni, mjumbe wa kamati ya heet amesema wamefanikiwa kupitia mitaala nane (8) katika ngazi mbalimbali na mitaala minne (4) mipya katika kampasi mpya za Babati na Songea
Ameongeza kuwa kikao hicho ni takwa la mradi wa heet ili kupitisha mapitio ya mitaala ambayo yamejumuisha maoni na mawazo ya wadau mbalimbali na wajumbe wa kamati.
Post A Comment: