Serikali wilayani Longido Mkoani Arusha katika kipindi cha miezi sita imefanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi bilioni 2.8 sawa na asilimia 93 ya bilioni 3.1 ya malengo ya makusanyo waliojiweke kama halmashauri kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Ufanisi wa makusanyo hayo unatokana na usimamizi wa thabiti wa maeneo ya kimkakati ya kikodi, udhibiti wa mianya ya ubadhirifu.
Mkuu wa Wilaya ya Longido Salumu Kali ameeleza hayo wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi, kwa kipindi cha Januari – Disemba 2024 kwenye Kikao cha CCM Wilayani humo.
Mapato hayo yanaonyesha Halmashuri ya Longido inapiga hatuo ya ukusanyaji, ukilinganisha na miaka mitatu iliyopita.
Wilaya ya Longido ilianzishwa mwaka 2007, ikimegwa kutoka wilaya ya Monduli, ikiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 8165.9, Wakazi zaidi ya laki moja na sabini na inapakana na Taifa Jirani la Kenya kupitia Mpaka wa Namanga.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Longido,Mheshimiwa Papaa Nakuata, amepongeza juhudi zinazofanywa na serikali katika kutekeleza Ilani ya chama huku akisisitiza kuwa chama kitaendelea kufuatilia kwa karibu utekelezaji wake.
“Tunaendelea kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa karibu ili kuhakikisha wananchi wa Longido wanafaidika na maendeleo tunayoyapigania,” amesema Mheshimiwa Nakuata.
Post A Comment: