Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa majaliwa akizindua kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya mama Samia mkoani Lindi 
Wananchi waliojitokeza 


Na Fredy Mgunda, Lindi.


Kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya mama Samia imezinduliwa rasmi katika mkoa wa Lindi kwa kuhakikisha wananchi wananufaika kwa kupata haki zao ambazo awali walikuwa wamenyang'anywa.


Akizungumza kampeni hiyo waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa majaliwa alisema kuwa kampeni hiyo imefanikiwa kutatua migogoro mingi iliyodumu kwa muda mrefu hadi hivi sasa.



Waziri mkuu alisema kuwa Kampeni hiyo imeongeza wigo wa utoaji haki kwa wananchi ambao walikuwa hawana uwezo wa kupata haki kwa kukosa fedha hivyo sasa kila mwananchi anapata haki bure.


Alisema kuwa huduma hiyo ya kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya mama Samia inatolewa bure bila malipo yoyote yale kwa kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suhulu Hassan.


Majaliwa alisema kuwa zaidi ya wananchi milioni 1.3  hadi sasa wamefikiwa na huduma hiyo huku wanaume wakiongoza kufika kupata huduma hiyo kuliko wanawake.


Aliwasisitiza wananchi wa mkoa wa Lindi kujitokeza kwa wiki kupata huduma ya kisheria kwa siku 9 kwenye kila wilaya na kufanikisha wananchi kupata haki zao.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: