Meneja kampasi ya Arusha IAA Dkt. Joseph Daudi amefunga rasmi mafunzo ya waandishi wa habari mtandaoni yaliyofanyika kwa siku mbili IAA

Akifunga mafunzo hayo Dkt. Joseph amewapongeza wanahabari walioshiriki na kusisitiza ni vyema wakayatumie mafunzo hayo kama sehemu ya kuboresha kile wanachokifanya katika tasnia ya habari kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla 

“Endeleeni kuwa wabunifu kwa kuyatumia mabadiliko makubwa ya teknolojia hasa matumizi ya Artificial Intelligence yaani AI kuleta mapinduzi katika tasnia yenu”amesema Dkt. Joseph

Dkt. Joseph ameongeza kuwa ni vyema wanahabari wakaendelea kutoa habari zenye ukweli na kuzingatia sheria hasa katika kipindi hiki tunapoelekea katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika November mwaka huu.

Kwa upande wake Mshiriki wa Mafunzo hayo kutoka Mwananchi Digital Ammar Masimba ameishukuru IAA kwa mafunzo hayo ambayo yamewajenga na kuwaongezea weledi katika tasnia hiyo na kwa kuwawezesha baadhi ya nyenzo ambazo watazitumia katika kazi yao.

Pamoja na mafunzo hayo IAA imetoa baadhi ya vitendea kazi na vyeti vya ushiriki kwa kila mwanahabari, huku wakiwapa fursa ya kutembelea sehemu mbalimbali Chuoni ikiwemo Jengo la library, Studio za IAA MEDIA, pamoja na Kiatamizi cha IAA Business Startup Centre (IBSUC) na kujionea huduma zinazotolewa na Chuo.























Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: