Muonekano wa sehemu ya Transfoma katika kitongoji cha Isenegeja Kijiji cha Isela kata ya Samuye Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Kijana aliyejulikana kwa jina la Daniel Mussa Mageni (27) mkazi wa Kitangili Manispaa ya Shinyanga amefariki dunia kwa kukosa hewa baada ya kupigwa na shoti ya umeme wakati akijaribu kuiba nyaya katika Transfoma iliyopo katika kitongoji cha Isenegeja Kijiji cha Isela kata ya Samuye Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Mashuhuda wanasema kuwa Daniel ambaye ni Fundi Umeme ,mkazi wa Kitangili Shinyanga Mjini,  aliyezaliwa Kilulu wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu amekutwa amefariki katika Transfoma iliyopo jirani na Zahanati ya Isela kata ya Samuye leo asubuhi Februari 24,2025, huku baiskeli aliyotumia kusafiria na vifaa alivyokuwa akivitumia kukata nyaya vikiwa eneo la tukio. 
Sehemu ya waya uliokuwa tayari umekatwa 

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Isegeneja, bi. Amina Hamis Bwire amesema mwanaume huyo amebainika kupoteza maisha dunia majira ya saa 12 asubuhi baada ya kupigwa na shoti ya umeme wakati akijaribu kujuhumu miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Mhandisi Mwandamizi wa TANESCO Mkoa wa wa Shinyanga, Anthony Tarimo akizungumza kwa niaba ya Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga amesema kijana huyo amefariki dunia wakati akiingilia njia ya umeme mkubwa katika Transfoma hiyo.

“Kitaalamu ameingilia njia ya umeme mkubwa, ameingilia usalama wa Transfoma akapata ajali hiyo. Alikuwa anajaribu kuiba nyaya za shaba zinazolinda usalama wa Transfoma”,ameeleza Mhandisi Tarimo.
Mhandisi Anthony Tarimo

Mhandisi Tarimo amewataka wananchi kuwa waangalifu na kuacha vitendo vya kuhujumu miundombinu ya umeme, akisisitiza kuwa ulinzi wa miundombinu hiyo ni jukumu la kila mmoja. 

“Ulinzi wa miundombinu ya umeme ni jukumu letu sote, toeni taarifa kuhusu wanaohujumu. Pia wananchi epukeni kusogea kwenye Transfoma na njia za umeme kwani ni hatari. Ukiangalia hata hapa kwenye hii Transfoma kuna onyo kabisa kwamba ni HATARI”,amesema Mhandisi Tarimo.

Amewahimiza wananchi kutoa taarifa pale wanapobaini uhujumu na uharibifu wa miundombinu na kuepuka kukaribia maeneo ya Transfoma, kwani ni hatari kwa maisha.

“Kwa upande wa usalama, miundombinu ya umeme ni hatari na tunapaswa kuepuka kujihusisha nayo kwa namna yoyote ile. Tunaomba wananchi wawasiliane na mamlaka husika pale wanapobaini watu wanaohujumu miundombinu,” ameongeza.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema Jeshi la polisi lilipata taarifa za kuwepo kwa tukio hilo majira ya saa 12 na nusu asubuhi katika kijiji cha Isela kata ya Samuye na kufika eneo la tukio ambapo mwananchi huyo anayesemekana kuwa ni Fundi umeme, amefariki dunia kwa kupigwa na shoti ya umeme wakati akijaribu kuiba waya wa Copper uliokuwa kwenye Transfoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi

"Mwili wa marehemu tayari tumeufikisha upo katika hospitali yetu ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya uchunguzi ili mwili ukabidhiwe kwa wanafamilia",amesema Kamanda Magomi.

"Tunakemea vitendo hivi, na hawa watu ambao aidha walishawahi kufanya kazi TANESCO au Vishoka, tunakemea vitendo hivi kwa sababu hii ni hujuma kwa miundombinu ya serikali. Serikali inafanya kazi kubwa sana ya kutoa fedha nyingi ili wananchi waweze kufikiwa na umeme, lakini wapo watu wachache ambao hawana mapenzi mema na nchi ya Tanzania ambao wanahujumu miundombinu ya umeme.

 Jeshi la polisi tuko imara na tunaenda kwenye Operesheni kali, endelevu kuhakikisha kwamba tunaendelea kulinda miundombinu yote ikiwemo ya Treni ya Mwendokasi SGR ili kuhakikisha pesa za watanzania zinatumika ipasavyo",ameeleza Kamanda Magomi.
Wakazi wa Isela kata ya Samuye Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakiangalia mwili wa Daniel Mussa Mageni (27) aliyefariki dunia baada ya kupigwa na shoti ya umeme alipojaribu kuiba nyaya katika Transfoma.
Wakazi wa Isela kata ya Samuye Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakiangalia mwili wa Daniel Mussa Mageni (27) aliyefariki dunia baada ya kupigwa na shoti ya umeme alipojaribu kuiba nyaya katika Transfoma.
Wakazi wa Isela kata ya Samuye Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakiangalia mwili wa Daniel Mussa Mageni (27) aliyefariki dunia baada ya kupigwa na shoti ya umeme alipojaribu kuiba nyaya katika Transfoma.
Muonekano wa sehemu ya Transfoma katika kitongoji cha Isenegeja Kijiji cha Isela kata ya Samuye Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya Transfoma katika kitongoji cha Isenegeja Kijiji cha Isela kata ya Samuye Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga

Muonekano wa sehemu ya Transfoma katika kitongoji cha Isenegeja Kijiji cha Isela kata ya Samuye Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya Transfoma katika kitongoji cha Isenegeja Kijiji cha Isela kata ya Samuye Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Share To:

Post A Comment: