Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko
akizungumza na Watanzania waishio India pamoja na watumishi wa Ubalozi
wa Tanzania nchini India mara baada ya kumaliza ziara nchini humo
zilioanza Februari 10 - 14, 2025 jijini New Delhi ( Februari 14, 2025)

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega mara baada ya kutembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini India zilizopo New Delhi Februari 14, 2025 jijini New Delhi

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko
(katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa
wanafunzi wanaosoma nchini India ambao alikutana nao akiwa ziarani
nchini humo Februari 14, 2025 jijini New Delhi. Wa pili kulia ni Naibu
Waziri wa Kilimo, David Silinde, Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe.
Iddi Kassim na Wa Pili kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini India,
Mhe.Anisa Mbega.


Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametembelea Ubalozi wa Tanzania nchini India na kuzungumza na
Watumishi katika ofisi hiyo.

Akizungumza katika Ofisi hizo jijini New Delhi, Dkt. Biteko amempongeza Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega kwa
mapokezi mazuri na kazi nzuri zinazofanywa na Ubalozi huo ikiwemo
kutangaza fursa za uwekezaji.

“ Nakushukuru kwa mapokezi mazuri mliyotupatia tangu tulipofika hapa kwa kweli yamerahisisha utekelezaji wa majukumu yetu, mnaipa heshima
kubwa Serikali kwa namna ambavyo Ofisi hii inavyohudumia watu
mbalimbali wenye uhitaji wanapokuja hapa ikiwemo watu wanaoonesha nia
ya kuwekeza Tanzania au Watanzania wanaotaka kuwekeza hapa India."
Amesema Dkt. Biteko

Amesema ushiriki wa Wizara ya Nishati katika Mkutano wa Wiki ya Nishati India umekuwa na manufaa mbalimbali ikiwemo kuhamasisha ushiriki wa wawekezaji mbalimbali katika duru ya tano ya kunadi vitalu
vya mafuta na gesi asilia.

Ameongeza kuwa " Kwa upande wa Wizara ya Nishati tutajitahidi watu wanapotoka India kuja Tanzania kama wawekezaji tuwape ushirikiano
mzuri,”

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Nishati na Madini, Mhe. Iddi Kassim amesema Kamati hiyo imefarijika
kwa kupata fursa ya kushiriki Wiki ya Nishati nchini India ambapo wamejifunza masuala mbalimbali na kupata uzoefu katika usimamizi wa
sekta ya nishati hasa ikitambulika kuwa India imepiga hatua kubwa
kwenye nishati.

Dkt. Biteko amemaliza ziara yake ya siku tano nchini humo ambapo anarejea nchini Februari 15, 2025.

Awali, Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbegai alimshukuru
Dkt. Biteko kwa ziara ambayo amesema kuwa imewaheshimisha kama mwenyeji wa Ujumbe wa Tanzania nchini India.

" Nitumie fursa hii kukupongeza kwa majukumu yako uliyotekeleza ukiwa
hapa na tunakushukuru kwa heshima kubwa uliyotupatia.” Amesema Mbega

Aidha, Mhe. Mbega ametaja baadhi ya majukumu ya Ofisi ya Ubalozi kuwa ni kuimarisha uhusiano baina ya nchi za uwakilishi, kulinda maslahi ya nchi na kuhakikisha fursa mbalimbali zinapatikana kama vile masoko,
Share To:

Post A Comment: