Na Fredy Mgunda, Lindi.
Katibu tawala wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Theresia Mtewele ameonya tabia ya baadhi ya wazazi kutowapa thamani sawa watoto wenye ulemavu na kuwatenga au kuwaficha kwa kuona kama laana kuzaa watoto wenye hali hizo.
Mtewele amesema Serikali imeweka mipango Madhubuti ya kudhibiti vitendo vya ukatili kwa watu kutoka makundi maalum na kutenga fedha kwa ajili ya kusaidia makundi haya katika Nyanja mbalimbali ikiwemo afya Pamoja na elimu.
Aidha Mtewele ameionya tabia ya baadhi ya wazazi kuwafanya watoto wenye ulemavu kitega Uchumi na kuwatembeza huku na kule wakiomba msaada badala yake wawasaidie kwa kuwawezesha kupata haki zao za msingi kwani wanaweza kutimiza ndoto zao kama watoto wengine
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama Vya Walemavu Kasulu Zakayo Nkohozi ameishukuru serikali kwa namna inavyoendelea kuwakumbuka na kuwashirikisha watu wenye mahitaji maalum katika shughuli mbalimbali na kuwapatia msaada mbalimbali kutatua changamoto wanazopitia ikiwemo kuwapatia vifaa wezeshi.
Aidha amesema huko nyuma walemavu walipuuzwa na kuonekana hawana uwezo wa kufanya chochote lakini serikali inaendelea kuwapa mafunzo yanayowawezesha kujitambua na kujihusisha katika shughuli mbalimbali za kiuchumi zinazowawezesha kupata kipato na hivyo
Post A Comment: