Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),CPA Anthony Kasore,alipotembelea banda la VETA katika Maonesho ya uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo kwa mwaka 2014, toleo la 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
Na.Alex Sonnna-DODOMA
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),CPA Anthony Kasore, amesema kuwa asilimia 80 ya mafunzo yatolewayo na VETA ni ya ujuzi na kwa maana hiyo ni mojawapo ya utekelezaji wa sera mpya ya Elimu ya mwaka 2024 toleo la mwaka 2023.
CPA Kasore ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la VETA katika Maonesho ya uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo kwa mwaka 2014, toleo la 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma amesema kuwa sera hiyo ambayo inalenga kufungua uchumi wa kijana wa kitanzania tayari imeisha anza kutekelezwa na VETA kwa kutoa elimu ya ujuzi kwa asilimia 80.
Aidha ameeleza kuwa katika kuhakikisha sera hiyo inafanya kazi kwa kiwango cha juu kwa sasa nchi ina vyuo 65 ambavyo vipo kwa ngazi ya wilaya huku VETA ikiwa na vyuo 80 kwa sasa .
Haya hivyo CPA Kasore amesema kuwa katika kuhakikisha elimu ya ujuzi inatolewa VETA inazingatia utoaji wa elimu ya ujuzi ambayo itakuwa na viwango vya kupata kazi kwa ngazi ya ukanda,kitaifa na kimataifa.
" VETA haikuwaacha watu wenye makundi mbalimbali kwani sera inalenga kuyafikia makumdi yote kwa lengo la kumpatia ujuzi mtu mmoja mmoja ,jamii na makundi yote kwa lengo la makundi hayo kupata ufanisi wa kujiongezea kipato kwa mtu mmoja mmoja au taifa kwa ujumla wake."amesema CPA Kasore
Pia ameelezea umuhimu wa sera mpya ya elimu na mitaala iliyoboreshwa amesema kuwa itasaidia vijana wa kitanzania kuingia katika soko la ajira na kwa kutumia teknologia kwa haraka tofauti na ilivyokuwa sasa .
" Sera hiyo ambayo Rais Samia ameizindua ni chachu ya maendeleo kwa taifa la Tanzania pamoja na mtu mmoja mmoja kwani kila atakayekuwa amemaliza elimu ya lazima atakuwa na ujuzi wa kumfanya aingie katika soko la ajira au kujiajiri mwenyewe."amesema
Katika kutoa ufafanuzi wa umuhimu wa kuwepo kwa sera hiyo amesema kuwa VETA itahakikisha kunakuwepo vyuo vya kutosha nchini ambavyo wananchi watapata fursa mbalimbali ya ufundi stadi na ujuzi kwa kusoma na kwa vitendo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),CPA Anthony Kasore,alipotembelea banda la VETA katika Maonesho ya uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo kwa mwaka 2014, toleo la 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
Post A Comment: