Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mh. Mibako Mabubu (Diwani) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi. Rose Manumba, wameongoza Kikao cha Baraza la Madiwani. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala tarehe 28 Novemba, 2025.
Katika kikao hicho waheshimiwa madiwani wamempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala pamoja na wataalamu kwa kazi nzuri za ukusanyaji wa mapato pamoja na usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Ndg.Fabian Kamoga amempongeza Mkurugenzi Mtendaji pamoja na madiwani kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato pamoja na ushirikiano mzuri walio nao kati ya watumishi na waheshimiwa madiwani hao. “Ninaawapongeza sana Mkurugenzi, Madiwani na timu nzima ya watumishi kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato. Ninawashauri kuzingatia mgawanyo wa fedha hizo kama miongozo inavyo elekeza”, Kamoga alisema.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Msalala Mh. Mboni Mhita amelipongeza Baraza la Madiwani kwa kazi kubwa linayoifanya katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala na kuwataka kuendelea kuwa wamoja na kuendelea kushirikiana na wataalamu katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuendelea kutoa huduma iliyo bora kwa Wanacnhi.
Pia madiwani wa Halmashauri hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wa wa Baraza hilo Mh.Mibako Mabubu wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kutoa fedha zinazoendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo ya Halmashsuri hiyo.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Bi. Rose Robert Manumba amewashukuru waheshimiwa madiwani kwa ushirikiano wao mkubwa wanaompatia pamoja na ushauri anaoupata kutoka kwa wataalamu. Aliendelea kusema kwamba ushirikiano wa unachochea kasi ya ukusanyaji wa mapato pamoja na usimamizi wa miradi inayo endelea kutekelezwa.
Pia Mkurugenzi Mtendaji amewataka wataalamu kuendelea kujituma katika utekelezaji wa majukumu yao ya kiutumishi pamoja na kutoa ushirikiano kwa waheshimiwa madiwani.
Kikao kimehudhuriwa na waheshimiwa madiwani, watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya msalala, wageni mbalimbali toka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, wananchi pamoja na viongozi wa vyama rafiki vya siasa na wadau toka Taasisi mbalimbali za Umma.
Post A Comment: