WAZIRI wa Katiba na Sheria Mhe Dkt Damas Ndumbaro ameeleza kuwa katika Mikoa 11 waliyopita katika Kampeni ya Mama Samia Legal Aid wamebaini maeneo manne yenye changamoto kubwa zaidi ikiwemo ukatili wa kijinsia pamoja kuwepo kwa Sheria ya makosa ya kujamiiana No.4 ya mwaka 1998 lakini bado kadhia hiyo ipo,pili Migogoro ya Ndoa,Mirathi, huku Migogoro ya Ardhi ikionekana kuongoza kwa kuonekana kuwepo kwa ubabaishaji na ujanja ujanja unaoelekea kwenye kwenye jinai.


Waziri Ndumbaro ameyaeleza haya mapema Leo hii Jijini Dodoma Januari 20,2025 katika mkutano wake na Waandishi wa habari wakati akielezea mwendelezo wa Kampeni hiyo katika Mikoa 6 ikiwemo Kigoma,Kilimanjaro, Geita,Katavi,Tabora na Mtwara inayoanza January 24,2025.

Na kuongeza kuwa program hiyo ya Mama Samia Legal Aid Campaign ni mkombozi kwa wanyonge wasiokuwa na uwezo wa kumudu gharama za Mwakili,wasio na uwezo gharama za mfumo mzima wa sheria kwanibkuna hata kulipia nyaraka moja ya Sheria hawezi.

"Baada ya kupita kwa Mikoa 11 tumebaini maeneo manne ndio yana changamoto kubwa zaidi,eneo la kwanza ukatili wa kijinsia bado ni changamoto pamoja na uwepo wa sheria ya makosa ya kujamiiana No.4 ya mwaka 1998 bado kadhia hii ipo,pili Ndoa Migogoro ya ndoa mambo ya taraka na mgawanyo wa mali,Mirathi ambapo katika hili suluhu ni kuandika Wosia japo watu wanaogopa kwa imani zao,eneo la nne no Ardhi tena hili ndo linaongoza ,tumegundua hiko kwenye Ardhi kuna ubaibaishaji mwingi na ujanja ujanja ambao unakwenda kwenye jinai,hivyo tutauomba Uongozi na Waziri wa Ardhi watuletee orodha ya Migogoro sugu ya ardhi ili tykishamaliza mikoa yote tutakwenda kuangazia kwenye Ardhi kwa kwenda kwenye eneo la tukio na kupambana nalo".

Aidha Waziri huyo amesema kuwa mpaka sasa Mama Samia Legal Aid Campaign katika Mikoa 11 ya mwanzo imewafikia Watanzania hasa wanyonge 775,119 ambapo asilimia 49 na wanawake na asilimia 51 ni wanaume na tayari kampeni imekwisha tatuta Migogoro 3162 kwa maana ya kuipokea,kusikiliza na kuitatua.

"Lakini mpaka sasa ninapoongea Mama Samia Legal Aid Campaign katika Mikoa 11 imeshawafikia Watanzania 775,119 ambapo asilimia 49 ya hao ni wanawake na asilimia 51 ni wanaume, imeshatatua Migogoro 3162 kwa maana ya kuipokea,kusikiliza na kuitatua,kwahiyo takwimu zinaonesha wanaume ni wengi kuliko wanawake, hivyo wapo watakaosema wanawake wanaogopa kujitokeza,wapo watakaosema wanaume ndo wananyanyasika sasahivi,tafsiri zinaweza kuwa tofauti ila takwimu ndio hizo".

Ameongeza kuwa asili ya mwanadamu ni kuwa na kiu ya haki jambo ambalo limekuwa gumu kwa Watanzania waishio vijijini ambao hawamudu kupata haki na msaada wa kisheria tofauti na wale waishio mijini ambako kuna huduma za misaada ya Kisheria ikiwemo Mahakama na Taasisi mbalimbali za utoaji wa msaada wa kisheria na wanamudu katika kupata haki hiyo.

"Ni asili ya mwanadamu kuwa na kiu ya haki,sasa wapo ambao wanamudu kupata haki hiyo kutokana na elimu yao na uwezo wa kiuchumi na wapi wanaishi kijiografia,kwahiyo mijini kupata haki ni nafuu kwasababu Taasisi nyingi za kuoata msaada wa kisheria ziko nyingi,Mahakama ziko nyingi mjini,wenzetu walioko vijijini hawa wana kiu ya kuoata haki".

Mpango huu ulianza April 2022 na mpaka sasa tayari umeenda Mikoa 11 na kuwafikia Watanzania wengi.
Share To:

Post A Comment: