Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Dkt Selemani Saidi Jafo amelipongeza Shirika la Maendeleo la Taifa(NDC) kwa kazi kubwa wanayo endelea kuifanya katika miradi mikubwa ya kimkakati. Dkt. Jafo aliyasema hayo alipokuwa akiongea na wananchi wa Kata ya Engaruka wilayani Monduli.
"Mkurugenzi wa NDC Dkt. Nicholas Shonde pamoja na watendaji wako kwasasa mnachapa kazi sana na hongereni sana" amesema Dkt. Jafo.
Shirika la NDC ndipo linalo simamia mradi mkubwa wa Magadi soda wa Engaruka ambapo kwasasa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fadha ya kulipa fidia wananchi wanaopisha mradi. Jimla ya fedha iliyotengwa kwaajili ya fidia ni shilingi bilioni 14.48 ambapo fedha zitakazolipwa kwa wananchi ni shilingi bilioni 6.2 na fedha nyingine itaelekezwa katika ujenzi wa miundombinu ya huduma za jamii kwa wananchi hao waopisha mradi.
Naye Mkurugenzi wa NDC, Dkt. Nicholas chonde ameuhakikishia uuma kwamba watazimamia vyema uwekezaji huo mkubwa ambao utaenda kuchochea uchumi wa Taifa la Tanzania.
Madini ya Magadi Soda ni muhimu sana katika viwanda vya vioo, nguo, sabuni, na viwanda mbalimbali.
Post A Comment: