Makamu Mwenyekiti wa tume huru ya taifa ya uchaguzi, Mheshimiwa Jaji (R) ( MST.) Mbarouk Mbarouk alisema kuwa ni kosa la jinai mwananchi kujiandikisha zaidi ya mara moja
kaimu mkurugenzi tume ya uchaguzi Giveness Aswile alisema kuwa Mkoa wa Lindi kutumia vituo 1308 kuandika wapiga kura katika daftari la kudumu la mpiga kura ikiwa ni ongezeko
kaimu mkurugenzi tume ya uchaguzi Giveness Aswile alisema kuwa Mkoa wa Lindi kutumia vituo 1308 kuandika wapiga kura katika daftari la kudumu la mpiga kura ikiwa ni ongezeko
NA Fredy Mgunda, Lindi.
Mkoa wa Lindi unatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 121,187 sawa na ongezeko la asilimia 18.7 ya wapiga kura 645,644 waliopo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura hivyo mkoa wa Lindi unatarajia kuandikisha wapiga 768,641.
Akizungumza wakati wa mkutano wa tume na wadau wa uchaguzi wa kuhusu uboreshaji wa daftari la wapiga kura,kaimu mkurugenzi tume ya uchaguzi Giveness Aswile alisema kuwa Mkoa wa Lindi kutumia vituo 1308 kuandika wapiga kura katika daftari la kudumu la mpiga kura ikiwa ni ongezeko
Awali akifungua mkutano huo, makamu Mwenyekiti wa tume huru ya taifa ya uchaguzi, Mheshimiwa Jaji (R) ( MST.) Mbarouk Mbarouk alisema kuwa ni kosa la jinai mwananchi kujiandikisha zaidi ya mara moja.
Jaji Mbarouk alisema kuwa ukibainika unaweza fungwa jela miezi sita au miaka miwili ili kujiepusha na kadhia hii hakikisha unajiandikisha mara moja tu.
Alisema kuwa Kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 10 Cha sheria ya Uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani Na.1 ya mwaka 2024,wafuatao hawana sifa za kuandikishwa kwenye Daftari,Iwapo mtu yupo chini ya kiapo Cha utii wa nchi nyingine tofauti na Tanzania,Hana akili timamu.
Aidha Jaji Mbarouk alisema mwananchi yoyote yule aliyewekwa kizuizini kama muhalifu mwenye ugonjwa wa akili,Amewekwa kizuizini kwa ridhaa ya Rais,Ametiwa hatiani kwa kosa ambalo adhabu yake ni kifo na anatumikia kifungo kwa kosa ambalo adhabu yake inazidi miezi sita iliyotolewa na mahakama.
"KUJIANDISHA KUWA MPIGA KURA NI MSINGI WA UCHAGUZI BORA"
Post A Comment: