Wananchi  wa Loliondo wilayani Ngorongoro na Simanjiro Mkoa wa Manyara wanatarajia kunufaika na huduma za mawasiliano kutoka kampuni ya Yas ambapo awali mawasiliano yalikuwa shida maeneo hayo ya pembezoni.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Januari 16, 2025 Ofisa Mkuu wa Biashara kutoka YAS, Isack Nchunda  amesema mabadiliko ya chapa ya kampuni hiyo yanakwenda sanjari na uboreshaji wa huduma za mawasiliano.

Amesema amesema hatua hiyo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Kanda ya Kaskazini amesema upelekeaji wa mawasiliano hayo haswa maeneo ya Loliondo na Simanjiro ni kuboresha huduma bora za mawasiliano.

“Tumefika maeneo yenye changamoto ya mawasiliano kwa kasi ya 4G na 5G lakini pia huduma zetu za tigo pesa sasa zinajulikana kwa Mixx by Yas ikiwemo kampeni yetu ya magift ya kigift ambayo wateja wetu wanashinda zawadi mbalimbali za fedha taslim pamoja na gari ”

Wakati huo huo, Kaimu Mkurugenzi wa Yas Kanda ya Kaskazini, Daniel Mainoya ameongeza kuwa kampeni ya “magifti ya kugift” bado inaendelea huku washiriki wakiendelea kujishindia zawadi za kila siku na kila wiki ikiwemo zaidi ya sh, milioni 156 na simu janja 172 zilizobakia.

Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: