Katibu Tawala Wilaya Mhandisi Zuhura Rashid kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya amezindua na kugawa Miche ya Minazi kwa Wakulima kutoka Kata ya Nkowe, Makanjiro, Malolo, Nandagala, Mandarawe, Mandawa, Mnacho, Chienjele, Ruangwa, Namichiga na Chibula.

Na Fredy Mgunda, Ruangwa.

Katibu Tawala Wilaya Mhandisi Zuhura Rashid  kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya  amezindua na kugawa Miche ya Minazi kwa Wakulima kutoka Kata ya Nkowe, Makanjiro, Malolo, Nandagala, Mandarawe, Mandawa, Mnacho, Chienjele, Ruangwa, Namichiga na Chibula.

Nazi ni zao la biashara na chakula katika Ukanda wa Pwani ambapo Minazi inaweza kustawi kwenye maeneo ya mwinuko wa chini karibu na mwambao wa Maziwa.

Kwa Wilaya ya Ruangwa imeanzisha Kitalu cha Miche zaidi ya 4,000 pia imepokea jumla ya Miche ya Minazi 7,000 ambapo upatikanaji wa Miche hiyo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa kwa wakulima katika Ziara yake aliyoifanya Septemba 18, mwaka 2023, alipotembelea Mkoa wa Lindi na kuwaahidi wakulima kuwa atawapatia wakulima Miche ya Minazi 50,000 kwa lengo la kuendeleza zao hilo.

Aina ya Miche ya Minazi iliyogaiwa kwa wakulima hao ni Miche ya Minazi mirefu ya asili ya East Africa Tall(EAT) ambayo huchukua muda wa miaka 5-7 toka kupandwa hadi kuzaa na ni aina nzuri, kubwa zenye kustahimili magonjwa na wadudu, na tija yake hufikia zaidi ya Nazi 45 kwa mti kwa mwaka na ina uwezo wa kuishi hadi miaka 70.

Aidha, Mhandisi Zuhura ametoa wito kwa wakulima waliopatiwa Miche hiyo kuitunza na kuilinda ili kufikia malengo

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: