Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Ntuli Kapologwe amesema  mtu anaponawa mikono ana uwezo wa kuzuia Maambukizi ya Magonjwa mbalimbali ya  mlipuko  zaidi ya asilimia 40  ikiwemo Marburg, Kipindupindu na Ebola na Magonjwa mengineyo.

Dkt. Kapologwe amebainisha hayo Leo tarehe 31, Januari, 2025  Wilayani Biharamulo Mkoani Kagera katika Ufunguzi  wa Mafunzo kwa  Timu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Afya Ngazi ya Mkoa na Halmashauri kuhusu ugonjwa wa Marburg yaliyoratibiwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani(UNICEF).

"Ni muhimu  jamii kuendelea kujenga desturi ya kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni kwani kufanya hivyo inasaidia kuzuia Magonjwa mbalimbali zaidi ya asilimia 40 ya Magonjwa hayo ya mlipuko kama vile Kipindupindu, Ebola na si Marburg pekee"amesema.

Aidha, Dkt. Kapologwe ametoa wito kwa timu hizo za usimamizi wa Afya kuweka Kipaumbele suala la utoaji wa Elimu ya Afya kuhusu ugonjwa wa Marburg.

"Lazima elimu yetu iwe kubwa katika kukabiliana na ugonjwa wa Marburg na nimefurahi sana kupata taarifa kuwa kila Halmashauri  inapata elimu na namba ya Wizara ya 199 imekuwa na mchango mkubwa, amesema.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma kutoka Wizara ya Afya Dkt. Ona Machangu amesema kuna umuhimu mkubwa wa Ushirikiano katika utoaji wa elimu ya afya.

Mratibu wa Huduma za Afya Ngazi ya Jamii kutoka Wizara ya Afya Dkt. Norman Jonas amesema ugonjwa wa Marburg  pia huchagiza mwili kushindwa kugandisha damu vizuri.

Kwa upande wake, Afisa Afya Mkoa wa Kagera Yasin Mwinory ametoa wito kwa Timu za Usimamizi wa Afya Ngazi ya Halmashauri kuweka Mpango Mkakati katika Utoaji wa Elimu ya Afya.

Kwa taarifa, Elimu na Ushauri zaidi Piga 199 Bure





















Share To:

Post A Comment: