Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga (wa tatu toka kulia) akikata utepe kuashiria kuzindua maadhimisho ya Wiki ya Sheria yaliyoanza Januari 25, yanatarajia kumalizika Februari 3, 2025 katika viwanja vya stendi ya zamani mjini Babati, Manyara.
Na Cathbert Kajuna- MMG/Kajunason Blog, Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga (pichani) ameiasa jamii kutunza amani na Utulifu kwani ndiyo nguzo ya maendeleo.
Hayo ameyasema wakati akizindua maadhimisho ya Wiki ya Sheria iliyoanza leo Januari 25, itamalizika Februari 3, 2025 yanayofanyika mjini Babati, Manyara.
Mhe. Sendiga amesema kuwa Watanzania wanatakiwa kuitunza amani maana ...panapokosekana amani mambo yanakwenda mlama hivyo ni vyema tupambane kuilinda amani yetu.
"Nasisitiza Watanzania wenzangu tuilinde amani yetu kwa gharama yeyote, angalieni nchi ambazo amani imekosekana wanavyohangaika na hazina maendeleo... kutwa kuchwa wananchi wamekuwa wakimbizi," amesema RC Sendiga.
Vile vile Mhe. Sendiga amewaasha wananchi kuacha kuhangaika hangaika kukimbilia mahakamani. Si kila jambo la linahusu mahakama mengine yanamalizika majumbani.
Amewasihi Watumishi wa mahakama na wadau ni wajibu kutenda haki
Kufanyakazi bila upendeleo, tuwatie moyo watumishi.
Awali akitoa elimu ya kisheria, Jaji Mfawidhi Kanda ya Manyara Mhe. John Kahyoza (pichani) amesema kesi zinazoongoza mahakamani ni masuala ya mirathi linalosababishwa na jamii kutokujua kuandika wosia.
"Naomba kuwaomba Watanzania wenzangu tuandike wosia ili kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima katika familia zetu, maana kesi nyingi mahakamani zinazoongoza ni masuala ya mirathi," amesema Mhe. Kahyoza.
Mhe. Kahyoza ameongeza kuwa wosia ni siri ya baba na mama hivyo ni vyema kushirikishana katika kuandika na si vyema mtoto akajua wosia huo ili kuondoa mafarakano.
Amesema ni vyema pia wasimamizi wa mirathi wakatambua wajibu wao ni Kukusanya mali za marehemu, Kulipa madeni na Kugawa mali kwa warithi watakapotekeleza wataepusha migogoro katika familia.
Kauli Mbiu: Tanzania ya 2050: Nafasi ya Taasisi zinazosimamia Haki madai katika kufikia malengo makuu ya dira ya Taifa ya maendeleo.

Post A Comment: