Jumla ya timu 120 zinatarajiwa kushiriki mashindano ya soka yanayojulikana kwa jina la Vunjabei Cup 2025 yatakayozinduliwa rasmi Januari 11 mwaka huu katika viwanja tofauti.

NA DENIS MLOWE IRINGA 


JUMLA ya timu 120 zinatarajiwa kushiriki mashindano ya soka yanayojulikana kwa jina la Vunjabei Cup 2025 yatakayozinduliwa rasmi Januari 11 mwaka huu katika viwanja tofauti.


Akizungumza na wanahabari, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Vunjabei Fadhil Ngajilo alisema kuwa awali yalifahamika kama Ngajilo Cup, sasa yameboreshwa kwa kiwango kikubwa, ambapo zawadi ya mshindi wa kwanza imeongezwa kutoka ng’ombe mmoja hadi shilingi milioni 10.


Ngajilo ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM mkoa wa Iringa alisema wameongeza zawadi kwa mshindi wa pili na wa tatu kutoka seti ya vifaa vya michezo hadi Sh Milioni tatu kwa mshindi wa pili na Sh Milioni mbili kwa mshindi wa tatu.


Aliongeza kuwa zawadi nyingine zitakuwa kwa kikundi bora cha ushangiliaji anbapo kitapata Laki  5 mwandishi bora (Magazeti, redio,tv na blog , mchezaji bora wa mashindano, mfungaji bora wa mashindano na kipa bora wa  wa mashindano.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Soka  Manipsaa ya Iringa, Yahaya Mpelembwa alisema wamejipanga kufanya ligi yenye ushindani mkubwa na michezo ya awali itachezwa kwa mtindo wa mtoano lengo kupata timu 50 bora ambazo zitacheza mtindo wa nyumbani na ugenini.

Alisema timu zitakazoingia kwenye 50 bora zitawezeshwa vifaa vyote vinavyohitajika kama jezi, mpira, soksi na viwanja vitavyotumika katika mechi za utangulizi ni viwanja vya kihesa, hoho , mlandege, ipogolo

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: