TANZANIA imeingia makubaliano na Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) kuipatia Serikali ya Tanzania mkopo wenye masharti nafuu kiasi cha shilingi bilioni 354.45, kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Uendelezaji wa Kilimo Vijijini unaojulikana kama “Agriculture and Rural Development Two Step Loan Project.

Mradi huu utatekelezwa chini ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) huku ukisimamiwa kwa karibu na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) kwa niaba ya Serikali ya Japan.

Akizungumza leo Januari 14, 2025 wakati wa kusaini mkataba huo Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema utekelezwaji wa mradi huu unaendana na Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano ambao una mahudhui ya kufikia ushindani na Uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya watu ili kuongeza tija na uzalishaji kwa kutumia rasilimali zilizopo.

Amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo utachochea ukuaji wa sekta ya kilimo kwa kuongeza uzalishaji kwa wakulima kupitia upatikanaji wa mitaji nafuu.

“Upatikanaji wa mitaji ya kilimo utawezesha pia wakulima kuwa na mazao mchanganyiko, na kuwa na kilimo kinachostahimili mabadiliko ya tabia nchi, ambako kutachangia usalama wa chakula, maendeleo vijijini na uhimara wa Uchumi kwa ujumla,” amesema Waziri Dkt. Nchemba.

Aidha amesema mradi huo unaendana na Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo ambao unalenga kuimarisha na kuchochea matumizi ya zana za kisasa za kilimo, usalama wa chakula na lishe, kuwezesha upatikanaji wa masoko, na kuwezesha uongezaji wa thamani.

“Hivyo, unaweza kuona jinsi ufadhili huu ulivyo wa muhimu. Napenda kuwahakikishia kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itachukua hatua zote muhimu kuhakikisha mradi huu natekelezwa kwa ufanisi, ili kufikia malengo yaliyokusudiwa,” amesema.

Pamoja na hayo Dkt. Nchemba ameishukuru na kuipongeza Serikali ya Japan kwa kuendelea kushirikiana katika kuendelea kuboresha maeneo muhimu ya maendeleo nchini.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Jica, Katsura Miyazaki Mradi huu unalenga kuchangia katika kuboresha tija ya kilimo na kuongeza mapato kwa wakulima na kuongeza thamani katika mnyororo wa mazao manne yaliyopewa kipaumbele.

“Mazao manne yaliyopewa kipaumbele ni mpunga, mahindi, ngano na alizeti iliyoorodheshwa katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa Serikali ya Tanzania FYDP III na itaimarisha mnyororo wa thamani na usalama wa chakula,” amesema.

Amesema pia fedha hizo zitagharamia sekta ya kilimo cha bustani na kutengeneza fursa za ajira kwa wanawake na vijana na kuimarisha ujumuishaji wa kifedha.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Mandeleo ya Kilimo Tanzania (TAdB), Frank Nyabundege amesema fedha hizo zitatolewa kwa riba ndogo ili kuwezesha wakulima wadogo waweze kumudu kuichukua ili waweze kulima kwa tija na kujiinua kiuchumi zaidi.

Amesema upatikanaji wa fedha hizo ni muendeleo wa yale yanayofanyika katika kilimo huku akisema tangu serikali ya awamu ya sita iingie madarakani zaidi ya Sh954 bilioni zimeelekezwa TAdB.

Nyabundege amesema fedha hizo ili kuhakikisha watanzania wengi wananufaika na kilimo kwa kuwatoa katika kilimo cha kujikimu kwenda cha biashara.

“Serikali imekuwa ikisaidia sekta ya kilimo ili iweze kufanya vizuri na wenzetu wanasema ukitaka kutajirila nenda katika kilimo,” amesema

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba (Katikati aliyeketi) na Balozi wa Japan nchini anayemaliza muda wake, Mhe. Yasushi Misawa (kushoto aliyeketi), wakisaini Hati za Mkataba (Exchange of Notes) kati ya Serikali ya Tanzania na Ubalozi wa Japan, wakati wa hafla iliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Hazina, jijini Dar es Salaam, ambapo katika hafla hio Mhe. Dkt. Nchemba alisaini Hati ya Mkataba mwingine wa mkopo wenye masharti nafuu kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) wa shilingi bilioni 354.45, kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Uendelezaji wa Kilimo Vijijini unaojulikana kama “Agriculture and Rural Development Two Step Loan Project”, utakaosimamiwa na JICA kwa niaba ya Serikali ya Japan na upande wa Serikali ya Tanzania utatekelezwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba (Katikati) na Balozi wa Japan nchini anayemaliza muda wake, Mhe. Yasushi Misawa (Kushoto), wakibadilishana Hati za Mkataba (Exchange of Notes) iliyosainiwa kati ya Serikali ya Tanzania na Ubalozi wa Japan, wakati wa hafla iliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Hazina, jijini Dar es Salaam, ambapo katika hafla hio Dkt. Nchemba alisaini Hati ya Mkataba mwingine wa mkopo wenye masharti nafuu kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) wa shilingi bilioni 354.45, kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Uendelezaji wa Kilimo Vijijini unaojulikana kama “Agriculture and Rural Development Two Step Loan Project”, ambao utasimamiwa na JICA kwa niaba ya Serikali ya Japan na upande wa Serikali ya Tanzania utatekelezwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba (Katikati aliyeketi) na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bi. MIYAZAKI Katsura (kulia), wakisaini Hati za Mkataba wa mkopo kati ya Serikali ya Tanzania na JICA wa shilingi bilioni 354.45, kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Uendelezaji wa Kilimo Vijijini unaojulikana kama “Agriculture and Rural Development Two Step Loan Project”, utakaosimamiwa na JICA kwa niaba ya Serikali ya Japan na upande wa Serikali ya Tanzania utatekelezwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB). Wengine katika picha wanaoshuhudia tukio hilo ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mhe. Fujii Hisayuki (wa pili kushoto aliyesimama), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi (wa pili kulia aliyesimama), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo (wa tatu kulia aliyesimama) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Bw. Frank Nyabundege.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba na Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bi. Miyazuki Katsura, wakionesha Hati za Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kati ya Serikali ya Tanzania na JICA wa shilingi bilioni 354.45, kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Uendelezaji wa Kilimo Vijijini unaojulikana kama “Agriculture and Rural Development Two Step Loan Project”, utakaosimamiwa na JICA kwa niaba ya Serikali ya Japan na upande wa Serikali ya Tanzania utatekelezwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, akizungumza wakati wa kusaini makubaliano ya mkopo wa shilingi bilioni 354.45 kutoka Serikali ya Japan kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Uendelezaji wa Kilimo Vijijini unaojulikana kama “Agriculture and Rural Development Two Step Loan Project”, utakaosimamiwa na JICA kwa niaba ya Serikali ya Japan na upande wa Serikali ya Tanzania utatekelezwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB). Hafla hiyo imefanyika leo Januari 14, 2025 Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Bw. Frank Nyabundege akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba wa mkopo kati ya Serikali ya Tanzania na JICA wa shilingi bilioni 354.45, kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Uendelezaji wa Kilimo Vijijini unaojulikana kama “Agriculture and Rural Development Two Step Loan Project”, utakaosimamiwa na JICA kwa niaba ya Serikali ya Japan na upande wa Serikali ya Tanzania utatekelezwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).

Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bi. Miyazuki Katsura akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba wa mkopo kati ya Serikali ya Tanzania na JICA wa shilingi bilioni 354.45, kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Uendelezaji wa Kilimo Vijijini unaojulikana kama “Agriculture and Rural Development Two Step Loan Project”, utakaosimamiwa na JICA kwa niaba ya Serikali ya Japan na upande wa Serikali ya Tanzania utatekelezwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mhe. Fujii Hisayuki akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba wa mkopo kati ya Serikali ya Tanzania na JICA wa shilingi bilioni 354.45, kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Uendelezaji wa Kilimo Vijijini unaojulikana kama “Agriculture and Rural Development Two Step Loan Project”, utakaosimamiwa na JICA kwa niaba ya Serikali ya Japan na upande wa Serikali ya Tanzania utatekelezwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).

Wadau mbalimbali wakifuatilia hafla hiyo.

Share To:

Post A Comment: