Na Denis Chambi, Tanga.
MDAU wa maendeleo Mkoani Tanga John Mapima ameiomba Serikali kuunda tume maalum itakayohusika na kuchunguza mienendo ya watumishi katika sekta mbalimbali hapa nchini ikiwemo sekta ya afya ambao wamekuwa wakikiuka miiko yao ya kazi ikiwemo kuwatolea lugha chafu wananchi pale wanapohitaji huduma.
Mapima ametoa ombi wakati akizungumza na vyombo vya habari ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu lilipotokea tukio la kujibizana baina yake na mtumishi mmoja wa hospitali ya wilaya Ngamiani iliyopo jijini hapa ( jina limehifadhiwa) baada ya kuhitaji msaada kiti mwendo wa kwaajili ya kumbebea mgonjwa aliyempeleka kupatiwa huduma siku hiyo.
Kwa mujibu wa Mapima amesema "Nilifika hospitali na mgonjwa nikapewa kiti mwendo ambacho ni kipya kwajili ya kumbebea mgonjwa wangu niliyempeleka lakini baadaye alitokea nurse mmoja ambaye hakunijibu vizuri alinijibu kwa kejeli na kudai kuwa kiti kile kina mwenyewe baada ya kumhoji majibu yake hayakunipendezesha na alienda ndani kuleta kiti kingine ambacho ni chakavu ili mgonjwa wangu aweze kuwekwa kwenye kiti hicho, tulilazimika kumbebea hivyo hivyo japo hali yake haikuruhusu kulingana na mazingira ya kile kiti ki ukweli Ile iliniumiza sana"
Kufwatia changamoto hiyo aliyokutana nayo ilimlazimu Mapima kwenda kununua kiti mwendo kingine na kukipeleka hositalini hapo ili kuweza kusaidia wahitaji wengine huku akiiomba Serikali pamoja na kuboresha mazingira pamoja na huduma nyingine kutazama hali hiyo ambayo bado uhitaji wake ni mkubwa.
"Nilijiuliza ni wagonjwa wangapi wanaofanyiwa kama mimi ki ukweli sikupendezwa hata kidogo baada ya huduma nikamrudisha mgonjwa wangu nyumbni kesho yake nilienda dukani kuulizia gharama ya kitimwendo kipya nikakinunua kwa shilingi 250,000 nikawapelekea nikakutana naganga mfawidhi wa kituo alinipokea vizuri tu" alisema.
"Katika hospitali za umma tunapitia changamoto nyingi sana watumishi waliofanya kazi kwa muda mrefu sehemu moja wanakuwa na mazoea kuna watu wanajibu wagonjwa vile wanavyojisikia wao ningeshauri iundwe tume ambayo itakuwa inapitia wale wafanyakazi waweze kutambua majukumu yao"alisema Mapima.
Pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ikiwemo kuboresha huduma hususani kwenye sekta ya afya Mapima amewaomba wadau wa Maendeleo kujitokeza kuchangia kwa hali na mali mahitaji mbalimbali.
" Napenda kuishauri jamii husasan wenzetu wenye uwezo wa kifedha kujitolea msaada wa vitu mbalimbali ambavyo vina umuhimu na uhitaji mkubwa kulingana na mazingira ili kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuwahudumia wananchi" alisisitiza
Post A Comment: