Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, ameongoza kikao cha tathmini ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 na maandalizi ya mbio hizo kwa mwaka 2025. Kikao hicho kimewakutanisha viongozi wa serikali, kamati za ulinzi na usalama, pamoja na wadau wa maendeleo ili kujadili mafanikio, changamoto, na mikakati ya kuboresha mbio zijazo.

Rc Mtaka amesisitiza umuhimu wa maandalizi madhubuti kuhakikisha Mwenge wa Uhuru 2025 unaleta matokeo chanya kwa maendeleo ya wananchi wa Njombe. Pia, amewataka viongozi wa halmashauri zote kushirikiana kwa karibu katika utekelezaji wa miradi inayotarajiwa kuzinduliwa au kukaguliwa na Mwenge wa Uhuru mwaka huu.

Mwenge wa Uhuru umeendelea kuwa chombo muhimu katika kuhamasisha maendeleo na mshikamano wa kitaifa, huku Mkoa wa Njombe ukiweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha mafanikio makubwa katika mbio zijazo.







Share To:

Post A Comment: