Katika kipindi cha miaka 4 (Machi, 2021 hadi Disemba, 2024) Serikali imeidhinisha jumla ya kiasi cha fedha za kitanzania 5.71 Billion kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 17 jimbo la Mchinga na Shilingi 12.79 billioni kwa ajili ya ya utekelezaji wa miradi 13 katika Halmashauri ya Mtama ikiwemo miradi 5 ya uchimbaji wa visima katika kila jimbo la uchaguzi kwa lengo la kuhakikisha kuwa Zaidi ya asilimia 85 ya wananchi waishio vijijini wanapata huduma ya maji safi na salama. kupitia kwa wakala wa maji safi na usimamizi wa mazingira wialaya ya Lindi (RUWASA).
Aidha wakazi 166493 wa Halmashauri ya Mtama watanufaika na mradi huo kwa halmashauri nzima na wakazi 71,174 wa Kata 10 za jimbo la Mchinga mchinga watanufaika na mradi huo.
Akiwa katika ziara ya kimkakati ya kukagua utekelezaji wa miradi ya ilani mkuu wa wilaya ya Lindi Victoria Mwanziva akiwa kwenye ziara hiyo ametembelea miradi miwili ya uchimbaji wa visima vya maji Dimba pamoja na kitongoji Cha Runyu kata ya Kitomanga.
Pia Mwanziva Amesema adhima ya Mh Raisi ya kutoa magari ya uchimbaji wa visima mia 900 vya maji katika kila Mkoa yanafanya kazi na visima hivyo vinachimbwa Ili wanainchi waweze kurahisishiwa kupata maji yaliyo safi na Salama.
Aidha Mkuu wa wilaya amewataka wahandisi na wasimamizi miradi hiyo mwili kukamilisha Mradi ndani ya siku 14 Ili wanainchi hao waweze kupata maji haraka Ili waweze kuondokana na adha ya kufuata maji umbali mrefu.
Post A Comment: